Mtuhumiwa Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’( katikati) aliyemuua mwanaye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey.
YULE mtoto
wa umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey aliyeuawa
kikatili kwa kunyongwa kisha kuzikwa na baba yake mzazi, Geofrey
Kilangwa ‘Simbaiwe’ (27) kwa kuwa alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake, amezidi kuibua maswali.Baadhi
ya wakazi wa Katavi waliozungumza na gazeti hili juzi, walihoji uhalali
wa baba kumjadili mtoto katika kuzaliwa kwa sababu ya kutanguliza
kiungo fulani.Wengine
walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri
kwa mwaka mmoja na miezi miwili? Mtuhumiwa ambaye pia ni mganga wa
kienyeji anayeishi Kitongoji cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma
wilayani Mpanda, alitenda unyama huo kwa madai kuwa mtoto huyo
alizaliwa akiwa ametanguliza makalio, hivyo ni nuksi kubwa katika
shughuli zake za uganga wa kienyeji, madai yaliyopingwa na watu
mbalimbali, zikiwemo taasisi za kutetea haki za binadamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, akizungumza na waandishi
wa habari mjini hapa, alidai mzazi huyo alitenda uhalifu huo Agosti
20, mwaka huu ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi, Agosti 26.
Ilidaiwa siku hiyo ya tukio,
mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake, alimzika kwa
siri katika kibanda chake anachofanyia shughuli za uganga.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
“Ndipo baba mzazi wa binti huyo alipomchukua marehemu na kwenda kumuuguza kwa siri
pasipo mama yake mzazi kufahamu kwani alimdanganya kuwa mtoto wao
amepelekwa kutibiwa na babu yake mkoani Mwanza,” alisema Kidavashari.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari,
wakazi wa kitongoji hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao, walimtilia
shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi zilizosambaa kwamba, Regina aliuawa
na baba yake mzazi na kuzikwa kwa siri.
Mwenyekiti huyo na wakazi wa eneo
hilo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake,
aliposhindwa kujibu wakasema wampekue ambapo alipinga vikali lakini alipopekuliwa kibandani kwake walibaini kuwepo kwa tuta dogo lililokuwa limechimbwa siku za karibuni.
Wakazi hao walifukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto Regina na ndipo wakalitaarifu jeshi la polisi.
Mama wa marehemu, Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Naye Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na mtuhumiwa, anadai kuwa alishirikishwa katika
maziko ya binti huyo baada ya kufa.“Hata hivyo, nilishtushwa sana kwa
kitendo cha mtuhumiwa kumzika mwanaye bila mkewe, nilipomuuliza akadai
mila za kwao mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio, mama mzazi wa
mtoto ni mwiko kushirikishwa katika maziko.
Kwa mujibu wa Kidavashari watu
wanne, wakiwemo wazazi wa marehemu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa mahojiano zaidi ambapo watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika.
Wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni
Regina Kaboni na Msolwa Jacob (29), mkazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe.
Source:GPL
0 blogger-facebook:
Post a Comment