Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani mkoani Mbeya huko wilayani Kyela baada ya magari mawili kugongana majira ya saa moja jioni katika maeneo ya Utengule katika jia ya Mbeya-Tukuyu.
Maafisa wa polisi wamewataja waliokutwa na mauti katika ajali hiyo kuwa ni Mortina mwenye miaka 30, Edina Jackson mwenye miaka 22, Paulo Mwanyalila ambaye ni Padri wa Kanisa Katoliki lakini pia ni paroko wa parokia ya Kyela, pamoja na mwanamke ambaye hakuweza fahamika jina.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi dogo aina yaToyota Coaster iliyosajiliwa kwa namba T. 241 BKZ lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika mara moja na gari ya pili ni ambalo halikufahamika ambapo baada ya kutokea tukio hilo watu wengine watatu walijeruhiwa ambao ni Samweli Asanga mwenye miaka 34, Mawazo Gasper pamoja na mtoto wa miaka kati ya 2-3 ambaye hakufahamika jina lake na madereva wote walikibia baada ya kusababisha ajali.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kinachunguzwa. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya na majeruhi pia wamelazwa hospitalini hapo.
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
0 blogger-facebook:
Post a Comment