Na Hudugu Ng'amilo KUTOKA NIPASHE ;
Ulaji wa kuku wa kisasa au broila' umeelezwa na wataalamu kuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maradhi ya saratani nchini.
Kitoweo
hicho kinasababisha kansa kwa vile ndege hao hulishwa vyakula kama
karanga, mahindi, mashudu na dagaa ambazo vina sumu ya 'mycotoxin'
inayotokana na fangasi ambayo inachochea ukuaji wa seli za saratani
mwilini.
Mshauri
wa Mifugo wa kampuni ya Bytrade Tanzania , Omari Magoma, alitoa
tahadhari hiyo katika mahojiano maalum ya NIPASHE Jumamosi, kuhusu
ugonjwa huo na kufahamisha kuwa tatizo la kansa ya kuku linaendelea
kuongezeka kila siku lakini likiwashambulia walaji na kukuza ukubwa wa
kansa nchini.
Alisema
ugonjwa huo ambao upo kwa muda mrefu kwenye miili ya kuku unasambaa
sehemu zote mwilini mwake na pindi mlaji anapokula kitoweo hicho mara
nyingi anaambukizwa maradhi ya kansa.
"Sumu ya
mycotoxin huzalishwa na fangasi kutoka kwenye chakula kama mahindi,
mashudu, karanga na dagaa vyakula ambavyo wafugaji huwalisha kukua ,"
alisema.
JAMII ZA FANGAS
Alibainisha kuwa, sumu hizo zina tabia tatu ambazo kusababisha kansa, kupunguza uwezo wa kuku kujikinga na maradhi ya kuambukizwa na kusababisha kuzaa viumbe wa ajabu.
Alibainisha kuwa, sumu hizo zina tabia tatu ambazo kusababisha kansa, kupunguza uwezo wa kuku kujikinga na maradhi ya kuambukizwa na kusababisha kuzaa viumbe wa ajabu.
Magoma
alitaja fangasi hao kuwa ni aspegilus wenye sumu ijulikanayo kitaalamu
kama aflatoxins b1 inayopatikana kwenye mahindi, mashudu, karanga na
dagaa.
Aina
nyingine ya fangasi ni 'penicillium' ambao wana sumu iitwayo ochratoxin
A. Japo fangas hawa wanatengeneza dawa kama peniciline au PPF ambayo
hutibu maradhi mengi wana sumu wanapotumiwa kwa utaratibu huo.
Fangasi
wengine kwa mujibu wa Magoma ni fussanum wenye sumu ya fumonisins T-2
hawa ni jamii ya fangas wanaoonekana kwenye nafaka zikiwamo mahindi
mchele na mtama.
UAMBUKIZAJI SARATANI
"
Kuku akila sumu hizi hupata kansa, kwa hiyo mwanadamu anaambukizwa
kutokana na mabaki ya sumu hizo zilizo kwenye mwili wa kitoweo hicho na
ataupata ugonjwa atakapokula mara nyingi nyama ya kukua" alionya.
Magoma
alisema sumu hizo hupatikana katika mazingira ya uzalishaji kama joto,
unyevunyevu unaoonekana kwenye mazao kuanzia utayarishaji mashambani
hadi matumizi majumbani.
Aidha,
kutokana na ukubwa wa tatizo mtaalam huyo aliwashauri wafugaji kutumia
dawa ya mycotoxin binder au check-o-tox inayokamata sumu na kuitoa
kupitia njia ya choo.
Alisema
moja ya kazi ya kirutubisho hicho ni kudhibiti sumu hiyo, kupunguza
unyevu kwenye chakula na huikusanya sumu kwenye mwili wa kuku kisha
kuitoa kwa njia ya haja.
Pia
aliwashauri wafugaji kununua vyakula vya kuku kwenye kampuni
zinazozalisha kwa viwango na wale wanaotengeneza wahakikishe wanaweka
kirutubisho hicho ili kukabiliana na tatizo la kansa ya kuku.
Magoma
alitaja dalili za ugonjwa huo kwa kuku kuwa ni mifuu yao kuwa na
madoadoa ya njano, ini lake kuwa kubwa zaidi na huwa na uvimbe kwenye
utumbo.
MFUGAJI AZUNGUMZA
Mfugaji
wa kuku mkazi wa jijini Dar es Salaam, Jonesia John alisema kutoka
aanze ufugaji kuku wake wamekuwa wakisumbuliwa na mafua ambayo yamekuwa
yakiwasababishia kuwepo kwa idadi kubwa ya kifo.
Alisema ugonjwa mwingine ambao umekuwa ukiwasumbua kuku wake ni homa ya tumbo.
Kuhusu kansa ya kuku, alisema amekuwa akisikia wafugaji wenzake wakilalamikia hilo lakini hajawahi kushuhudia kuku mwenye nao.
Hata
hivyo, alipoulizwa kama ana elimu yoyote ya ugonjwa huo ili pindi mifugo
yake itakapopata aweze kukabiliana nao, alisema mara nyingi amekuwa
akinunua vyakula salama vya kuku kwenye kampuni.
0 blogger-facebook:
Post a Comment