728x90 AdSpace

­
Latest News
August 18, 2014

MBUNGE WA TEMEKE AZIDI KUFANYA MAMBO MAKUBWA JIMBONI MWAKE

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ameendelea kumwaga misaada kwa wadau na makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo lake, Pichani, Mtemvu akizungumza kabla ya kuanza kugawa zawadi hizo kwa ambao hawakuzipata wakati wa Mfungo uliopita wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, zaidi ya wananchi 900 walipata zawadi hizo alizogawa jana kwenye viwanja vya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
 Mtemvu akionyesha chupa ya chai ambayo ni miongoni mwa seti za vifaa vya nyumbani alivyozawadia wananchi katika hafla hiyo.
 Mtemvu akimkabidhi mgawo wake, Tatu Ligalwike
 Mtemvu akimkabishi zawadi yake, Mohammed Mbonde, ambaye sasa ni Mjumbe wa Baraza la wazee wa CCM Temeke, ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM katika mikoa mbalimbali ukiwemo wa Shinyanga.
 Wadau kabla ya kukabidhiwa zawadi hizo
 Wadau wakiwa wamekaa kwenye madawati mapya kabla ya kupewa zawadi hizo, Katika hafla hiyo Mtemvu alikabidhi pia madawati 100 kwa viongozi wa Kata mbili ikiwemo ya sandali
Mtemvu akikabidhi madawati 50 kwa Diwani wa Kata ya Sandali Abel Tarimo. Jumla  13, zimeshanufaika na msaada wa mawati wa Mbunge huyo.Picha na Bashir Nkoromo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MBUNGE WA TEMEKE AZIDI KUFANYA MAMBO MAKUBWA JIMBONI MWAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown