728x90 AdSpace

­
Latest News
August 18, 2014

MH. SUMAYE ASHAURI KUSITISHWA KWA BUNGE LA KATIBA

Waziri mkuu wa zamani nchini Tanzania Fredrick Sumaye amependekeza kusitishwa kwa mjadala wa katiba mpya unaoendelea mjini Dodoma kwa kuwa inaonekana dhahiri kuwa si muda muafaka wa kupata katiba mpya kwa sasa.
 

Amesema kusitishwa kwa mjadala huo kutatoa fursa kwa watanzania kujipa muda zaidi wa kutafakari ili kufanikisha upatikanaji wa katiba muafaka kwa wakati unaofaa.
 

Kauli hiyo ya waziri mkuu wa zamani imekuja wakati bunge hilo linaendelea na vikao vyake mjini Dodoma vinavyohudhuriwa na wajumbe wengi kutoka chama cha Mapinduzi CCM.
 

Wakati huo huo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umesema Rais Kikwete ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi suala la kusitisha Bunge Maalum la Katiba na siyo mtu mwingine.
 

Umoja huo pia umeendelea na msimamo wa kumtaka Rais kuwasiliana na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kulisitisha bunge hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MH. SUMAYE ASHAURI KUSITISHWA KWA BUNGE LA KATIBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown