Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (pichani),ameunda kamati
ndogo yenye ujumbe wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala
ambayo hayakufikia muafaka wakati wa majadiliano ya kupitia sura
mbalimbali za Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.
Kamati
hiyo itakuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samia
Suluhu Hassan,ambapo wajumbe wa kamati hiyo wametoka kila pande ya
Muungano yaani watano wametoka Tanzania Bara na watano kutoka
Zanzibar.
Aidha
Mhe. Sitta akizungumzia kuhusu maendeleo ya kazi za Kamati hizo,
ambapo alisema zinaendele vizuri, hivyo kuanzia wiki ijayo sura zote 15
zitakuwa zimepigiwa kura,hivyo Kamati hizo zitakuwa zimemaliza sura 17
ya rasimu hiyo na za nyongeza ifikapo Agosti 27,mwaka huu ili kuanza
kuwasilisha katika Bunge hilo kuanzia Septemba 2,mwaka huu.
Hayo
yalisemwa leo na Mhe. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa
habari alipokutana nao leo kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya
Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo kutathmini kazi za Kamati 12 za
Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi ya mapendekezo ya kuongeza
Ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati zao.
Mwenyekiti
huyo aliyataja mambo ambayo yatashughulikiwa na kamati hiyo, ni muundo
wa Bunge katika masuala ya Muungano, uraia pacha, mahakama ya kadhi
na kamati ya pamoja ya fedha.
“Haya mambo manne nimeagiza ufanyike utaratibu maalum,” alisema Mhe. Sitta.
Mhe
. Sitta akizungumzia kuhusu tathimini ya mwenendo wa Kamati hizo,
alisema zipendekeza masuala kadhaa na kuacha mengine kama yalivyo
katika rasimu hiyo.
Akizungumzia
kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge
hilo,kabla ya kukutana na waandishi wa habari, Mhe. Sitta alisema kamati
hiyo imepokea mapendekezo kutoka katika kamati mbalimbali kuhusu
kuongezeka kwa sura na Ibara za rasimu hiyo.
Aliyataja
mapendekezo hayo , likiwemo la Tume ya Marekebisho ya Katiba
lililowasilisha na Jaji Warioba kuhusu ardhi, mazingira na rasilimali za
taifa, Jumuia ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) na pendekezo la
Haki ya Watumiaji huduma na bidhaa ili kuwalinda walaji lililowasilishwa
, Hawa Ng’umbi ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo.
Aliyataja mapendekezo mengine ni
la Jukumu la Serikali kujenga uchumi imara, ambapo lengo ni kuwa na
maendeleo ya uchumi wa ujamaa na kujitegemea na Kuwepo kwa Baraza la
Habari, la wajumbe wa 201 kuhusu ardhi, wafugaji, wavuvi pia na
wachimbaji wadogo ili ziweze kutungwa Sheria za kusimamia masuala hayo.
Mhe. Sitta alisema kutokana na mapendekezo hayo kutakuwepo na ongezeko la ukurasa na sura kadhaa katika rasimu hiyo.
Alisema
Kamati imebaini tatizo la mahudhurio, aliwapongeza wajumbe wa Bunge
hilo kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa na mahudhurio mazuri kwenye
vikao kuliko kutoka Tanzania Bara kuacha visingizio vya kutohudhuria
vikao.
Katika
hatua nyingine Mhe. Sitta alisema kutakuwepo na wataalamu kabla ua
kumalizika kwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa
kutoka Hazina kwa pande zote za Muungano, ambapo ataukuwepo pia Gavana
wa Benki Kuu, Profesa Bonaventure Rutinwa kwa ajili ya suala la uraia
pacha, uhamiaji na Profesa Issa Shivji ambaye ataoa ufafanuzi juu ya
aina ya Muungano ili kuwa na uwiano kwa kuwa hivi sasa yapo mambo
machache.
0 blogger-facebook:
Post a Comment