Mtoto mwenye umri wa
miaka 9 aliyefahamika
kwa jina la Nelly Alick
mkazi wa Mlolo amefariki dunia muda mfupi
wakati anapatiwa
matibabu katika hospitali
ya wilaya ya Mbozi baada
ya kugongwa na gari
lenye namba za usajili
T.257 CRP aina ya Toyota
Noah lililokuwa
likiendeshwa na Lameck
Madihan (34) mkazi wa
Mlolo.
Ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa 09:30
alasiri huko maeneo ya
Karasha, kata na tarafa
ya Vwawa, wilaya ya
Mbozi, mkoa wa Mbeya
katika barabara ya
Mbeya/Tunduma. Chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo
kasi.
Mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika
hospitali ya wilaya Mbozi.
Dereva amekamatwa na
gari lipo kituoni.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mbeya kamishina
msaidizi mwandamizi wa
polisi Ahmed Z. Msangi
anatoa wito kwa
madereva kuwa makini
wanapotumia vyombo vya
moto ili kuepuka ajali
zinazoweza kuepukika.
Aidha, anatoa wito kwa
watembea kwa miguu
kuwa makini
wanapotumia barabara ili
kuepuka madhara
yanayoweza kuepukika.
0 blogger-facebook:
Post a Comment