Jipya! Baada
ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa
staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The
Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya
mwandishi wet amenasa kinachoendelea. |
Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi
umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi
hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi (open) na
kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es
Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa
mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa
tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha
kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.
Wakili maarufu Bongo anayemtetea 'Lulu', Peter Kibatala.
YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari
zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao
cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha
ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama
ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi
kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza
kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza
kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye
kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.
ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi
wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa
mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa
mahakamani.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda
anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye hupenda
kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada
ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu
Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo
ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya
kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili
Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni
mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina
ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi
na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.
“Ni
kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi
huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini
nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili
na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata Lulu
haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala
aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop,
Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari
wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo,
mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama
aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba
aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki dunia
April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha Kanumba
kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa
ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya
Kinondoni, Dar.
0 blogger-facebook:
Post a Comment