Watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa al-Shabaab waliuvamia msafara wa
magari yaliyokuwa yakisafirisha mirungi kwenye Kaunti ya Lamu, na
kumkata kichwa msaidizi wa dereva na kuyateka magari mawili, Kamishna wa
Kaunti ya Lamu Miiri Njenga aliiambia Sabahi siku ya Jumatatu (tarehe
25 Agosti).
Njenga alisema magari hayo mawili yalikuwa yanasafirisha mirungi
kuelekea Somalia kupitia Lamu pale yaliposhambuliwa kwenye msitu wa
Bodhai wiki iliyopita.
"Kulikuwa na watu wanne kwenye magari hayo wakati walipoamriwa kuingia
msituni," alisema.
"Watatu waliachiwa na watekaji nyara wao siku ya Jumanne (tarehe 19
Agosti). Mtu wa nne, jina lake kwenye kitambulisho chake ni George Mwiti
kutoka Kaunti ya Meru, alipatikana amekatwa kichwa siku tatu baadaye."
Mwili na kichwa vilipatikana kwenye eneo la Kiunga katika msitu wa
Bodhai.
Chanzo: Sabahi.
0 blogger-facebook:
Post a Comment