Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, Kombe la Kagame, Azam FC
ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa
kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3
dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.Wachezaji
ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini
wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio
walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango Mwadin Ally kufanya kazi
nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao.
Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliajiLionel Saint- Preux kutoka Haiti.
Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon JosephMarious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mnokuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumona aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.
Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penalti, lakini
hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na
Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga
mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila
shaka.
0 blogger-facebook:
Post a Comment