MFANYABIASHARA
maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akisimikwa kuwa Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi
cha miaka mingine mitano na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye
uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Mwigulu Nchemba akizingumza na umati wa watu katika viwanja vya mwembetogwa
mwishoni mwa wiki mjini Iringa
MFANYABIASHARA
maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akizungumza na Wananchi mwishoni mwa wiki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi
cha miaka mingine mitano na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye
uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Salim Abri Asas akiwa na Wazee wa Kimila kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi
cha miaka mingine mitano.
Shughuli za kusimikwa zikiendelea huku wanahabari wakiendelea kurekodi tukio hilo.
Na Denis
Mlowe,Iringa
MFANYABIASHARA
maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas mwishoni mwa wiki amesimikwa kuwa Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi
cha miaka mingine mitano na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara
Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa,
mjini Iringa.
Akimuapisha
Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu
Mkuu wa CCM alisema analitumikia taifa hili akijua sehemu kubwa ya wananchi
wake ni masikini na lengo kubwa ni kuwaondoa katika lindi la umaskini.
Nchemba
alisema nchi inaliwa na moja ya eneo linalowaweka katika kazi kubwa ya
mapambano ni fedha zinazotolewa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo
ambazo hazitumiki ipasavyo na watendaji kwa kuzitumia katika miradi isiyo
endelevu na kusababishia nchi kutokuwa na maendeleo.
“Kuna
mambo mengi yanatokea katika halmashauri zetu kwasababu ya kukosa usimamizi
unaosababisha watu wetu wakose hali ya kupata huduma zinazotakiwa kutekelezwa
katika miradi ya maendeleo hivyo nitahakikisha kuwabana na kuwafuatilia kwa
kila halmashauri kuleta mchanganuo wa fedha jinsi zilivyotumika na kuhakikisha
mradi umekamilika na sio kusema kiasi Fulani kimetumika.” Alisema
Nchemba.
Aliongeza
kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuwasaka, kuwakamata na hatimaye
kuwafikisha katika vyombo vya dola watumishi wa umma wanaokula kodi za wananchi
kwa mikono miwili bila kunawa.
Mwigulu
alisema mambo mazuri yanakuja na serikali itaendelea kutengeneza sera
zinazojali watanzania ili keki ya taifa iliwe na watanzania wote na kudhibiti
matumizi ya ovyo na fedha tutakazokuwa tunatoa hatutaruhusu zitumike kwa kazi
tofauti na ile iliyokusudiwa.
Akimpongeza
Asas kwa kuwa kamanda wa UVCCM, Alisema UVCCM wakitimiza wajibu wao ipasavyo
watasaidia kupunguza maadui wakubwa wawili wa CCM ambao wameendelea kuwa na athari
kubwa wakati wa chaguzi za serikali.
Aliwataja
maadui hao kuwa ni pamoja na kujiingiza kwenye makundi ya wagombea na hila
zinazosababisha baadhi ya wana CCM wasitendewe haki stahiki kwenye vikao muhimu
vya chama.
Kwa
upande wake Kamanda Salim Asas alisema baada ya kuapishwa kwa kipindi kingine
lengo ni kuwainua vijana kiuchumi na kutaka ushirikiano katika kuleta maendeleo
ya wananchi wa mkoa wa Iringa bila kujali itikadi ya vyama na dini.
0 blogger-facebook:
Post a Comment