728x90 AdSpace

­
Latest News
August 21, 2014

BOMU LARUSHWA NDANI YA BASI NA KULIPUKA, ABIRIA WATATU WAFARIKI DUNIA HUKU SITA WAKIJERUHIWA KIGOMA.

Picha ya maktaba bomu likiwa limetegwa ardhini.

KIGOMA. Watu watatu wamekufa akiwepo mtoto mchanga na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria (Hiace) kurushiwa bomu na watu wasiojulikana huko Kasesema, Kigoma alfajiri ya leo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Buhigwe (OCD), Samwel Utonga alisema basi hilo lilikuwa likotokea Kilelema kwenda Kasulu Mjini ambapo watu hao walilirushia kitu kinachoaminika kuwa ni bomu.

Taarifa kutoka Hospitali ya Muyama zinazema majeruhi hao wamehamishwa toka hospitalini hapo na kupelekwa Hospitali ya Kasulu baada ya hali zao kuwa mbaya.


Chanzo: MWANANCHI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: BOMU LARUSHWA NDANI YA BASI NA KULIPUKA, ABIRIA WATATU WAFARIKI DUNIA HUKU SITA WAKIJERUHIWA KIGOMA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown