Natumaini kuwa si mgeni sana na jina hili la Kofii Olomide hususani kwa kile kizazi cha 2000's kushuka chini na hasa hasa wale vijana wazamani kwenye miaka 1990's.
Koffi Olomide ni msanii mkubwa wa muziki wa Dance wengi upenda kuuita "Lingala" kutoka huko nchi ya Demokrasia ya Congo.
Jina kamili la mwana'lingala huyu ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, maarufu kama Koffi Olomide
alizaliwa miaka 58 iliyopita (Julai 13, 1956) siku ya Ijumaa huko
Kisangani Demokrasia ya Congo. Jina hilo la Koffi alipewa na mama yake
mzazi akiwa na maana ya kuzaliwa kwake siku hiyo ya ijumaa (Friday).
Koffi amezaliwa na kukulia kwenye familia ya hali ya kawaida ikiwa na
maana kwamba familia yao haikuwa ya juu kiuwezo wa ya chini (middle
class - Family)
Alianza kujifunza kuimba na kuandika mashairi akiwa na umri mdogo na
kuwashangaza majirani zake hususani umahiri wake wa kutunga mashairi na
kupiga gita.
ELIMU: Koffi aliweza kubainika na baadhi ya wanafunzi wenzie na
walimu wake kuwa ni miongoni mwa wanafunzi wenye akili sana darasani na
kuweza kubahatika kupata scholarship ya kwenda kusoma huko Bordeaux
nchini Ufaransa, ambako alichukua degree yake ya Biashara na Uchumi.
Koffi alireportiwa kuwa ana'hold masters ya degree ya Hesabu
aliyochukulia huko Paris, kwenye chuo cha Paris University, nchini
Ufaransa.
Koffi alirudi nchini Kondo mnamo mwaka 1970's na kuweza kujiunga na Band
ya Papa Wemba, Viva la Musica, alianza kama mtunzi na mwandishi katika
band hiyo na muongozaji wa sauti pia. Mnamo mwaka 1986 Koffi alianzisha
band yake aliyoipa jina la Quartier Latin, ambayo imeweza kusherehekea
uwepo wake wa miaka 20 mnamo mwaka 2006.
0 blogger-facebook:
Post a Comment