JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Mhandisi Msose Michael
(35) mkazi wa Mkaongo Juu Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuwalawiti
mabinti wawili katika Kijiji cha Zogowale wilayani ya Kibaha.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa huo, Athumani Mwambalaswa alithibitisha
kukamatwa kwa mhandishi huyo na kusema aliwalawiti mabinti hao wenye
miaka 12 na 16 kwa nyakati tofauti.
Alisema mtuhumiwa huyo aliwachukua mabinti hao kutoka Nachingwea kwa
nyakati tofauti na kukaa nao nyumbani kwake jijini Dar es Salam kwa
ajili ya kufanya kazi za ndani.
Alisema baada ya siku kadhaa, aliwahamishia kwenye shamba lake
lililopo Zogowale kwa ajili ya kutunza mifugo yake na kwamba alikuwa
akilala nao chumba kimoja pindi alipowatembelea.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, wananchi walioshuhudia kitendo hicho
walitoa taarifa polisi ambao waliweka mtego na kumnasa mtuhumiwa huyo.
“Baada ya mtuhumiwa huyo kuwekwa chini ya ulinzi, mabinti hao ambao
walipelekwa katika kituo cha afya Mlandizi kupimwa na kugundulika kwamba
walilawitiwa hivyo kuanzishiwa matibabu,” alisema kamanda huyo.
0 blogger-facebook:
Post a Comment