Watu
wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Land Cruser
ilikuwa imebeba maiti 10 zikitokea hosiptali ya taifa Muhimbili kwenda
hospitali ya St Francis Ifakara kugonga wapanda pikipiki katika eneo la
Mtego wa simba Mikese mkoani Morogoro
Gari lililosababisha ajali toyota Land Cruser
Mwili wa mmoja waliofariki katika ajali hiyo
Pikipiki iliyosababishiwa ajali na kutoa uhai wa watu wawili waliokuwa wanakwenda shamba
Akizungumzia
tukio hilo kwenye eneo la tukio mkuu wa kikosi cha usalama barabarani
Bonifasi Mbao amesema gari hiyo ikiendeshwana dereva Pankrasi Pasco
mkazi wa ifakara iliwagonga wapanda pikipiki Shaban Rajab na Ally Benulo
wakazi wa Mikese na kufariki dunia papo hapo na chanzo cha ajali
mwendo kasi na dereva anashikiliwa na jeshi la polisi, kuhusu maiti 10
zilizokuwemo katika gari hiyo amesema zilikuwa zikipelekwa hospitli ya
St Fancis Ifakar kwa lengo la kufanya utafiti na mafunzo ambapo
wanafanya mawasilino ya kuzifikisha katika hospitali hiyo.
Nao
wananchi walioshuhudia tukio hilo wameeleleza chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi huku wakilalamikia matukio ya ajali nyingi katika eneo hilo
kutokana na kona na kuomba serikali kuweka matuta na vibao vya
tahadhari.
0 blogger-facebook:
Post a Comment