Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt Natalia Kanem akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM) Kushoto ni Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga na kulia ni Mtaalamu
wa Programu za Vijana kutoka UNFPA, Tausi Hassan.
*********
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI
Kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo imeahidi kukuza
na kuboresha misingi ya kuwashirikisha vijana katika utekelezaji wa sera
mbalimbali, programu na mikakati ya maendeleo.
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, Bibi Sihaba Nkinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya vijana
duniani kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bibi Venerose
Mtenga amesema kwamba lengo la kuwashirikisha vijan ni kuhakikisha kuwa
sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.
“Katika
kutekeleza eneo hili Tanzania inalenga kuweka fursa zitakazowawezesha
vijana kukuza utaalamu na ujuzi utakaowawezesha kufanikiwa katika
kipindi cha mpito kutoka ujana kwenda katika utu mzima,” amesema Bibi
Mtenga.
Amesema
kwamba Tanzania kama sehemu ya dunia inatambua changamoto maalum
zinazowakabili vijana walioko katika mazingira hatarishi pamoja na
umuhimu wa kuhakikisha kuwa vijana wanahusishwa kikamilifu katika
malengo ya maendeleo.
Bi
Mtenga aliongeza Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vijana
pamoja na wadau wa maendeleo ili kuunga mkono programu za elimu ya afya
kwa vijana walioko ndani na nje ya shule.
Alilisitiza
kwamba Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wataendelea
kuunga mkono taasisi za mafunzo rasmi na zisizo rasmi ili kukuza uwezo
na uelewa miongoni mwao katika masuala ya afya ya akili na mwili kwa
ujumla.
“siku
ya vijana duniani inatambua na kuthamini kuwa kipindi cha ujana
kinaambatana na mabadiliko makubwa na ya haraka na safari ya kutoka
utotoni kufikia utu mzima,”
“Safari
hiyo inaweza kuwa ngumu na yenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji
utulivu na ukomavu wa akili, hapa Tanzania, kwa mujibu wa Sera ya Taifa
ya Maendeleo ya vijana, kijana ni mtu yeyote mwenye umri kati ya miaka
15 hadi 35,” aliongeza.
Amesema
kwamba katika takwimu za kitaifa hapa nchini nusu ya idadi ya watu ni
vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Mgeni
Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi
Venerose Mtenga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya
kimataifa ya vijana duniani, kushoto kwake, ni Mwakilishi wa UNFPA, Dkt.
Natalia Kanem.
Bibi
Mtenga aliendelea kusema kwamba msisitizo mkubwa unawekwa katika
kuhakikisha vijana wanakuwa na fikra chanya ambazo ni za kimaendeleo na
zinazoleta mabadiliko chanya kwa jamii.
Kwa
Upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem
amesema kwamba siku ya vijana duniani ni nafasi nyingine kwa vijana
kukutana pamoja na kujadiliana matatizo na changamoto mbalimbali
wanazokabiliana nazo.
Amesema
kwamba vijana kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa katika kupambana na changamoto za matumizi ya pombe kupita
kiasi, dawa za kulevya na mimba za utotoni.
“kwa
pamoja serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya
kimataifa wana wajibu wa kushirikiana na vijana katika kuwasaidia
kufikia malengo yao mbalimbali katika harakati za kujiletea maendeleo,”
amesema Dkt. Kanem.
Dkt
Kanem aliongeza kwamba ni muhimu kwa vijana kutambua kwamba bila kuwa
na afya nzuri ya akili ni vigumu kupiga hatua za kimaendeleo na
kuondokana na umaskini wa kipato.
Amesema
kwamba katika mkutano unaokuja wa viongozi duniani watatumia nafasi
hiyo kuwakumbusha viongozi wa dunia umuhimu wa kuwekeza kwa vijana kama
taifa la kesho.
Dkt.Kanem
alifafanua umuhimu wa vijana na jamiii kwa ujumla kutumia mitandao ya
kijamii katika kupashana habari za afya ya uzazi na mambo yanayowahusu
vijana kwa ujumla.
0 blogger-facebook:
Post a Comment