728x90 AdSpace

­
Latest News
August 24, 2014

WAZIRI AAMUA KUVUA SUTI NA KUSAIDIA MAJERUHI,ATOA HUDUMA YA KWANZA


Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.

Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi zao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: WAZIRI AAMUA KUVUA SUTI NA KUSAIDIA MAJERUHI,ATOA HUDUMA YA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown