Kiongopzi wa Kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei |
Iran imetangaza jumatatu nia yake ya "haraka ya kuwapa silaha”
Wapalestina kwa kulipiza kisasi uamzi wa Israel wa kupeleka ndege isiyo
na rubani, ambayo kwa mujibu wa Tehran, imedunguliwa ikiwa katika anga
yake.
"Sisi tuko mbioni kuwapa silaha Wapalestina ili waweze kutetea eneo la
Cisjordania na tunajizuia kutoa maelezo yoyote kuhusu kutumwa kwa ndege
hiyo iliyodunguliwa, wakati ilikua ikikaribia eneo letu la kuzalisha
uranium la Natanz", amesema mkuu wa majeshi ya anga ya Iran,
Amir-Ali-Hajizadeh, kwa mujibu wa taarifa ziliyonukuliwa na mtandao wa
jeshi la Iran, Sepahnews.com.
Walinzi, amboa ni wanajeshi wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran wamefahamisha
kwamba wamedungungua ndege ya upelelezi ya utawala wa kizayuni ambayo
ilikua ikijaribu kukaribia eneo la nuklia la Natanz", ameongeza
Hajizadeh.
Jeshi la Israel likihojiwa na shirika la habari la AFP, limefahamisha
kwamba haliwezi kuzungumza chochote kuhusu taarifa za vyombo vya habari .
"Iwapo kitendo hicho kitajirudi, hatutosita kujibu haraka
iwezekanavyo", amesema Hajizadeh. .
Iran, ambayo haitambuwi kuwepo kwa taifa la Israeli, imekua ikiwapa wapiganaji wa kipalestina wa Hamas ambao wana mamlaka kamili katika ukanda wa Gaza pamoja na kundi lingine la Islamic Jihad, mafunzo ya kutosha kuhusu teknolojia ya kutengeneza makombora yanayotumiwa kwa kurusha katika miji ya Israeli yakitokea Palestina.
Mwishoni mwa mwezi Julai wakati jeshi la Israel lilikua limezidisha
mashambulizi katika ukanda wa Gaza, kiongozi wa kidini wa Iran,
Ayatollah Ali Khamenei, aliwatolea wito Wapalestina kuendelea mapambano
ya silaha kwa lengo la kudhibiti eneo la Cisjordania.
0 blogger-facebook:
Post a Comment