Mchezaji wa
Kimataifa wa Kenya, Allan Wanga, Leo Agosti 24,2014 huko Kigali, nchini Rwanda
ameipa Timu yake ya El Merreikh ya Sudan Ubingwa wa Klabu za Afrika Mashariki
na Kati na kutwaa Kagame Cup 2014, baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Wenyeji APR waliokuwa wakishuhudiwa na Rais Paul Kagame kwenye uwanja wa Amahoro.
Bao hilo la
ushindi la Wanga lilifungwa katika Dakika ya 24 na kuwapa El Merreikh Kombe na
kitita cha Dola 30,000.
APR
imeambulia Dola 20,000 kwa kushika nafasi ya pili.
|
0 blogger-facebook:
Post a Comment