Bomba la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es
Salaam Tanzania hadi Nchini Zambia lijulikanalo kama TAZAMA
limetobolewa na mafundi waKampuni ya Raddy Fiber Solution Ltd ya jijini
Dar es Salaam wakati wakichimba chini ya barabara kupitisha awamu ya
pili ya kebo za mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Gongo la
Mboto jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni ya Raddy, Rajab Mikumwo amesema
mafundi wake walitoboa bomba hilo kwa bahati mbaya majira ya saa nane
alasiri leo wakati wakifanya kazi ya kuchimba njia ya kupitisha bomba. Sehemu inayoonesha mafuta ya kimiminika baada ya bomba hilo kutobolewa chini.
Wakazi wa Gongo la mboto wake kwa waume wakiwa katika pilika za kuchota mafuta hayo machafu ya Diseli.
0 blogger-facebook:
Post a Comment