Kocha Diego Simeone ameizungumzia mechi ya kesho na kusema wapinzani wake, Real Madrid wameimarika zaidi.
Simeone
amesema Madrid wameimarika zaidi kupitia kiungo wao mpya Toni Kroos,
raia wa Ujerumani ambaye atafanya mechi hiyo izidi kuwa ngumu.
Kroos
amejiunga na Madrid akitokea Bayern Munich na alicheza katika mechi ya
Super Cup ya Ulaya dhidi ya Sevilla ambayo walishinda kwa mabao 2-0,
yote yakipachikwa na Ronaldo.
Timu
hizo zinakutana katika mechi ya Super Cup ya Hispania ambaye
huwakutanisha bingwa wa La Liga na Copa del Rey ikiwa ni maalum ya
kufungua msimu.
Pia alisema, mshambuliaji Gareth Bale amezidi kuwa bora kuliko msimu uliopita, hali ambayo itaongeza ushindani zaidi.
Washambuliaji: "Tunaendelea
kucheza kwa aina ya mtindo wetu hata kama tutakuwa hatuko na wachezaji
wote, ni mmoja tu, Diego Costa ndiye tutamkosa. Ila Jiménez yuko fiti na
anatufanya tuamini kama hakuna tatizo.”
Goalkeepers: "Moyá atacheza, pia Oblak ambaye yuko fiti, hivyo hatuna hofu. Kwa kifupi tuko tayari kwa ajili ya mechi hiyo."
0 blogger-facebook:
Post a Comment