728x90 AdSpace

­
Latest News
March 1, 2017

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransisko wa Kwaresma 2017


“NENO NI ZAWADI. NAFSI NYINGINE NI ZAWADI.” 

Ndugu wapendwa,

Kwaresima ni mwanzo mpya, njia ambayo inatuongoza kwenye lengo la Pasaka, ushindi wa Kristo juu ya kifo. Kipindi hiki tunaitwa kuongoka. Wakristo wanaitwa kumrudia Mungu “kwa mioyo yao yote” (Yoel 2:12) kukataa kwa kuishi katika hali mbili (uvuguvugu) na kukuwa katika urafiki na Bwana. Yesu ni rafiki Mwaminifu asiye tuacha sisi. Hata tukitenda dhambi anatusubiri kwa subira turudi kwake, kwa hali hii ya uvumilivu na subira anatuonesha utayari wake wa kusamehe (ref. Homilia januari 2016).

Kwaresima ni kipindi kizuri cha kuzama ndani zaidi juu ya maisha yetu ya kiroho kwa njia ya utakaso tunaopewa na Kanisa: kufunga, sala na kutoa sadaka. Kwa msingi wa vyote ni neno la Mungu, ambalo kwa kipindi hiki tunaitwa kulisikiliza na kuingia ndani zaidi. Ninataka sasa tutafakari juu ya mfano wa Tajiri na Lazaro maskini (rej. Lk 16:19-31) tutafute mafundisho katika mfano huu, kwani unatupa hali ya kuelewa kitu ghani tufanye ili tuweze kupata furaha na uzima wa milele na kwamba unatuvuta tufanye mabadiliko ya kweli ya wongofu.

1. Mwenzangu ni zawadi. 

Mfano unaanza kwa kuwonesha hawa wahusika wawili. Huyu maskini anaelezwa katika hali ya upana zaidi: ni dhaifu na anakosa hata nguvu ya kusimama. Amelala katika mlango wa tajiri. Anajishibisha kwa makombo yalio dondoka katika meza ya tajiri. Mwili wake umejaa vidonda na mbwa wanakuja kuvilamba vidonda vyake (mstari 20-21), taswira hii ni ya huzuni sana; inamuonesha huyu mtu akiwa katika hali ya ukiwa na huruma.

Kitendo hiki kinaeleweka zaidi kwamba hata huyu maskini jina lake ni Lazaro: jina lililo jaa ahadi, ambalo maana yake ni “Mungu anasaidia”. Tabia hii sio ya wote. Sifa zake zinaelezeka na kuonekana kama mtu aliye na historia yake. Wakati katika hali ya kawaida tajiri hatuioni, tunaona na kutambua kama mtu ambaye yupo karibu tu. Anakuwa sura, na kwa njia hiyo, ni zawadi, thamani kubwa, mwanadamu ambaye Mungu anampenda na kumjali, tofauti na hali yake halisi kama mtu asiye shikika (rej. Homilia Januari 8, 2016).

Lazaro anatufundisha kwamba kila mtu ni zawadi. Uhusiano sahihi na watu wengine unajaa utambuzi wa thamani yao. Hata maskini aliye katika mlango wa tajiri sio asieyafaa, bali wito wakuitwa kuongoka na kubadilika. Mfano huu unatuita tufungue moyo wa mioyo yetu kwa wengine kwasababu kila mtu ni zawadi, awe jirani yetu au awe mtu maskini. Kwaresima ni kipindi kizuri cha kufungua milango kwa wote walio wahitaji na kutambua ndani yao sura ya Kristo. Kila mmoja wetu anakutana na watu kama hawa kila siku. Kila maisha tunayo kutana nayo ni zawadi inayohitaji kuikubali, heshima na upendo. Neno la Mungu linatusaidia kufungua macho yetu kukaribisha na kupenda maisha hasa wakati yakiwa ni madhaifu na hali mbaya. Lakini ili kufanya haya lazima kufanya tunayo ambiwa na Injili kuhusu huyu tajiri.

2. Dhambi inatupofusha. 

Mfano huu haufichi mchanganyo uliofanywa na huyu tajiri (mstari wa 19) tofauti na maskini Lazaro, tajiri hana jina, anaitwa tu “Tajiri” utajiri wake unaonekana wa hali ya juu na wa mavazi ya thamani. Nguo za zambarao zilionekana za thamani kuliko za dhahabu na silva, na zili hifadhiwa kwa watu wa dini tu (rej 10:9) na wafalme (rej, Waamuzi 8:26), wakati zile zilizofumwa vizuri zilimpa mtu anaonekane kuwa na tabia ya kitakatifu. Huyu tajiri alikuwa ameathirika na utajiri wake, na tabia ya kuuonesha kila siku: “Alifanya sherehe kwa anasa kila siku” (Mstari 19). Ndani yake tunaweza kuona picha ya uharibifu wa dhambi, unakuwa kwa kupitia hatua tatu: kupenda pesa, ubatili na majivuno (rej, Homilia Septemba 20, 2013).

Mtume Paulo anatuambia kwamba “kupenda pesa ni mzizi wa dhambi” (1Tim 6:10). Ni chanzo cha ufisadi na wivu, mahangaiko na kujionesha. Hela zinaweza zikatutawala sisi, kiasi kwamba zaweza kutufanya tuwe wanyanyasaji. (reje Evangelii Gaudium 55). Badala ya kuwa kwetu chombo cha kuonesha huduma nzuri kwa wenzetu na mshikamano kwa wengine, hela zinaweza kutufunga sisi na ulimwengu kwenye kutokufikiri ambapo hakuachi nafasi ya upendo na amani.

Mfano unaonesha kwamba uchoyo wa huyu tajiri ulimfanya bahili. Nafsi yake ilitafuta tu kujionesha na kuonesha wengine kwamba anaweza kutenda. Bali muonekano wake wa nje ulifunika utupu wa ndani. Maisha yake ni gereza la maisha ya kuonekana, maisha ya juu juu na maisha yasio ya kweli (rej.ibidi., 62).

Hatua ya chini katika hali hii ya maadili ni majivuno. Tajiri huyu alivaa kama mfalme na kutenda kama ‘mungu’, akisahau kwamba yeye ni mwanadamu tu. Kwa wale walio haribiwa na kupenda mali, hakuna cha thamani isipokuwa nafsi zao. Walio karibu yao hawawezi kuingia katika mambo yao. Matokeo ya kujikita kwenye pesa tu ni aina ya upofu. Huyu tajiri hakumwona maskini aliyekuwa akiteseka kwa njaa, akiumia, akilala katika mlango wake. Kwa kuangalia tabia hii, tunaelewa kwanini Injili inalaumu kupenda fedha. “hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili: kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kutumikia Mungu na mali.” (Mt 6: 24).

3. Neno ni zawadi.

Injili ya tajari na Lazaro inatuandaa tufanye maandalizi mazuri ya Pasaka. Lirtujia ya Jumatano ya Majivu inatuita kukutana na hali kama hii ya tajiri. Wakati Padre anapotupaka majibu kichwani, anatamka maneno :”Kumbuka wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi”. Ukitazama, tajiri na maskini wote walikufa, na sehemu kubwa ya mfano inaongelea maisha baada ya maisha haya. Wahusika wote wawili ghafla wanatambua “hatukuleta kitu duniani, na hatukuchukua chochote kutoka duniani” (1Tim 6:7).

Sisi pia tunaona kinacho tokea katika maisha yajayo. Pale tajiri anaongea na Abrahamu kwa kirefu, anayemwita ‘Baba’ (Lk 16:24-27), kama alama kwamba yupo katika watu wa Mungu. Hali hii ya undani inafanya maisha yake yaonekana kuwa na matata, kwani mpaka sasa hakuna kilichosemwa kuhusu uhusiano wake na Mungu. Kwa uhalisia ni kwamba, hakukuwa na nafasi ya Mungu katika maisha yake. Yeye alikuwa ‘mungu’ peke yake.

Tajiri anatambua kuwa ni Lazaro pekee ameepuka tufani ya maisha baada ya kifo. Anataka maskini Lazaro ampooze kwa tone la maji. Anacho mwomba Lazaro kinafanana na kile ambacho yeye mwenyewe alishindwa kumtimizia Lazaro. Abrahamu anamwambia “kipindi cha maisha yako ulikuwa na sehemu yako ya vitu vizuri, kama Lazaro alivyokuwa na vitu vyake katika hali mbaya. Sasa ana farijika hapa wakati wewe ukiwa katika mateso” (mtari 25). Katika maisha yajayo, hali ya usawa inaletwa tena na maisha mabaya yana linganishwa na wema.

Mfano huu unaelendelea na kuleta ujumbe kwa wakristo wote. Tajiri anamuuliza Abrahamu amtume Lazaro kuwaonya ndugu zake walio hai bado. Lakini Abrahamu anamjibu “ Wanayo Musa na manabii wawasikilize wao. (mstari 29). Anaongeza tena kusema “kama hawataweza kuwasilikiliza Musa na manabii, hawata amini hata kama mtu akifufuka kutoka wafu” (mstari 31).

Tatizo la tajiri sasa linakuwa limejitokeza. Chanzo cha matatizo yote ilikuwa kwasababu hakusikiliza neno la Mungu. Na badala yake akakuwa bila kumpenda Mungu na akamtenga jirani yake. Neno la Mungu lii hai na lina nguvu, lina uwezo wakuwaongoa watu na kuwarudisha kwa Mungu. Tunapo fungua mioyo yetu kusikiliza zawadi ya Neno la Mungu, tunaishia kufungua mioyo yetu kwa jirani zetu.

Marafiki wapendwa, kipindi cha kwaresima ni kipindi cha kufanya maisha yetu upya na Kristo, kuishi katika neno lake, katika Sakramenti na jirani. Bwana wetu aliyeshinda vishawishi vya shetani wakati wa kufunga kwa siku arobaini, inatuonesha njia ambayo tunapaswa kuifuata. Tunaomba Roho Mtakatifu atuongoze katika njia sahihi ya kuongoka, ili tuweze kutambua zawadi ya neno la Mungu, tutakaswe na dhambi zinazo tupofusha, na kumtumikia Kristo katika ndugu zetu walio wahitaji. Ninawatia moyo Wakristo wote waonesha hali hii ya mabadiliko ya kiroho kwa kujali kampeni za Kwaresima sehemu mbali mbali za kanisa ulimwenguni, na hivyo kuwa na tamaduni za kujaliana katika familia hii moja ya Kibinadamu. Tuombeane ili, kwa kushiriki katika ushindi wa Kristo, tuweze kufungua milango yetu kwa ajili ya walio dhaifu na maskini. Na hivyo tutakuwa tayari kushiriki na kushirikishana furaha kamili ya Pasaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: Ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransisko wa Kwaresma 2017 Rating: 5 Reviewed By: Unknown