728x90 AdSpace

­
Latest News
March 11, 2017

TAFAKARI YA KWARESIMA: Kutamani Kuwa Mkamilifu


“KWARESIMA YA UKARIMU”
Jumamosi, Machi 11, 2017,
Juma la 1 la Kwaresima

Kumb 26: 16-19;
Zab 119: 1-2, 4-5, 7-8;
Mt 5: 43-48

KUTAMANI KUWA MKAMILIFU!

Liturujia ya leo inalenga katika Sheria ya Mungu, ambayo Mungu ametupa kwa njia ya Musa ili kuifuata kwa moyo na nafsi nzima. Katika Injili, tunaona Yesu, analeta upendo wenye athari kubwa, zaidi kuliko wowote ule ambao waliutenda kabla. Kumpenda kila mtu, bila kuwa na fikra au sababu yeyote ile, bila kujali kama wao wanatupenda sisi au la, bila kufikiria wanatuwazia mabaya au mazuri?
Yesu wakati alipokuwa dunia hii, alikabiliwa na upinzani sana, kutoka kwa mamlaka ya kidini, kutoka kwenye mamlaka ya kisiasa, kutoka mji wake mwenyewe, kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe. Hata hivyo, yeye amewapenda daima wote. Ujumbe wake wa huruma au wa kubadilika mara zote ulijawa na upendo mkuu. Hata juu ya Msalaba, aliwatazama kwa huruma watesi wake. Upendo kwa Mungu na kwa jirani huenda pamoja, na hauwezi kutenganishwa. Mt. Yohane anaweka wazi kwamba, “Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo (1Yoh 4:20). 

Leo tunapewa changamoto na upendo huu wa Yesu Kristo. Tumekuwa mara nyingi sana watu ambao tunabagua wengine, juu ya rangi, dini, jinsia, kabila, juu ya tabaka, utaifa, juu ya hadhi ya jamii, utamaduni, elimu, kiasi cha mali ulicho nacho nk, Je, tunaweza kuamua kumwiga Yesu kuanzia sasa na kuendelea? Je, tunaweza kuwapenda wale wote ambao wametuumiza katika maisha yetu? Wale wanaotutesa kwasababu ya utamaduni wetu, dini yetu,au mawazo yetu? Yesu alishinda haya yote kwa upendo wake, Je, sisi twaweza kufanya hivyo tushinde kwa njia ya upendo?

Sala: Bwana, ninataka kuwa mtakatifu. Ninataka kuwa mtakatifu kama wewe ulivyo mtakatifu. Nisaidie niishi kila wakati kwa ajili yako. Ninatoa muda wangu wote kwa ajili yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Tabia Takatifu ya Kwaresima: KUFIKIRI NA KUONGEA-Bwana nisaidie nijifunze KUFIKIRI kabla ya KUSEMA. Ninaomba niweze kutafakari kila kitu ninacho sema, na hivyo, kuachana na maneno yeyote yanayo waumiza wengine. Amina.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: TAFAKARI YA KWARESIMA: Kutamani Kuwa Mkamilifu Rating: 5 Reviewed By: Unknown