728x90 AdSpace

­
Latest News
March 15, 2017

KWA WANAUME: Zifahamu Sifa 7 za mwanamke wa Kuoa (Wife Material).


Na. James Waibina
Habari ndugu msomaji wa makala zangu katika blog hii ya Fumbuka, karibu tena siku ya leo tuweze kujifunza zaidi kuhusu Ndoa na Mahusiano, leo tutazungumzia  Mahusiano  hasa kwenye baadhi ya Sifa za Mwanamke wa kuolewa.

Mahusiano ni sehemu kubwa sana katika kufanikiwa au kutokufanikiwa kwenye maisha yako, kama hauko kwenye mahusiano mazuri unaweza kukuta ndoto zako zinakufa na unashindwa kuwa yule mtu ambae umepanga kuwa kwenye maisha yako, lakini pia kama ukiweza kuyatumia mahusiano vizuri pia yanaweza kuwa sehemu ya kufanikiwa kwenye maisha yako.

Hii ni hatua pekee ya kuweza kufanya uchaguzi mzuri wa yupi anayekufaa kuambatana naye na kuwa wamoja katika maisha namaanisha Ndoa.

Wapo watu wanaopenda raha tu katika maisha pasipo kujua kwamba kuna shida pia, Watu hawa ni wale wanaodhani maisha ni raha tupu na kwamba wanaoishi kwenye shida ni wajinga. Ukweli hauko hivyo, maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna siku mambo yanaweza kuwa si mazuri lakini siku nyingine mambo yakawa mazuri. Mwanamke wa kuoa lazima ajue hivyo.

Zifuatazo ni baadhi ya Sifa za Mwanamke anayestahili kuolewa :-

1. Hana Tamaa za Pesa 
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife material’.

2. Hayuko Tayari Kukuona Huna Amani

Mwanamke ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikishaanakurudisha kwenye hali ya kawaida, huyo anafaa kuwa mkeo.

3. Anapenda Watoto 
Utajuaje kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo.

4. Heshima Kwa Kila Mtu 
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.

5. Anajishusha
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, nawewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.

6. Anakuongoza Kwenye Mema
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.

7. Anajua Maisha Na Mapenzi 
Mapenzi yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke anayekufaa wewe ni yule ambaye anakupenda kwa dhati kabisa lakini pia anajua maisha. 

Maisha yanachangamoto nyingi sana ambazo wanandoa wanapaswa kushirikiana katika kuzitatua hivyo uchaguzi wa mwenza wako wa ndoa lazima ufanyike kwa makini katika hatua ya mahusiano kwa kumpata mtu anayejua maana ya maisha.

Ahsante.
Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia
0713515059  -Text /Call/WhatsApp au  jameswaibina@fumbuka.co.tz
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: KWA WANAUME: Zifahamu Sifa 7 za mwanamke wa Kuoa (Wife Material). Rating: 5 Reviewed By: Unknown