728x90 AdSpace

­
Latest News
March 26, 2017

MASOMO YA MISA: Jumatatu, Juma la 4 la Kwaresima Mwaka A- Tarehe 27/03/2017

SOMO 1
Isa. 65:17-21

Bwana asema: Tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.
Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 30:1, 3-5, 10-12 (K) 1

(K) Nitakutukuza, ee Bwana, kwa maana umeniinua.

Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua,
Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
Umeniinua nafsi yangu,
Ee Bwana, kutoka kuzimu.
Umenihuisha na kunitoa
Miongoni mwao washukao shimoni. (K)

Mwimbieni Bwana zaburi,
Enyi watauwa wake.
Na kufanya shukrani.
Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,
Katika radhi yake mna uhai.
Huenda kilio huja kukaa usiku,
Lakini asubuhi huwa furaha. (K)

Ee Bwana, usikie, unirehemu,
Bwana, uwe msaidizi wangu.
Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;
Ulinivua gunia, ukanivika furaha.
Ee Bwana, mungu wangu,
Nitakushukuru milele. (K)

SHANGILIO
Eze. 33:11

Sikufurahii kufa kwake mtu mwovu, asema Bwana, bali aiache njia yake mbaya, akaishi.

INJILI
Yn. 4:43-54

Baada ya siku mbili hizo Yesu aliondoka huko, akaenda Galilaya. Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe. Basi alipofika Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.
Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, jana, saa saba, homa ilimwacha. Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile alipoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

1 blogger-facebook:

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Item Reviewed: MASOMO YA MISA: Jumatatu, Juma la 4 la Kwaresima Mwaka A- Tarehe 27/03/2017 Rating: 5 Reviewed By: Unknown