728x90 AdSpace

­
Latest News
September 7, 2014

DAMU YA WATU WALIOPONA UGONJWA WA EBOLA KUTUMIKA KUTIBU WAGONJWA WENGINE




Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wamepona ugonjwa wa Ebola inaweza
kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine. Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.

Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.
Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana.


Chanzo:BBC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: DAMU YA WATU WALIOPONA UGONJWA WA EBOLA KUTUMIKA KUTIBU WAGONJWA WENGINE Rating: 5 Reviewed By: Unknown