728x90 AdSpace

­
Latest News
March 25, 2017

MASOMO YA MISA: Ijumaa, Juma la 3 la Kwaresima Mwaka A Tarehe 24/03/2017



SOMO 1
Hos. 14:2-9

Bwana asema: Ee Israeli, mrudie Bwana, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. Chukueni maneno pamoja nayi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo tutakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe. Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaimbia tena kazi ya mikono yutu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.
Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. Nitakuwa kama umande kwa Israeli; naye atachanua maua kama nyinyoro, na kuieneza miziz yake kama Lebanoni. Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni.
Na wao wakaao chini ya uvuli wake w2atarejea; watafufuka kama ngano, na kuchanua maua kama mzabibu; harufuyake itakuwa kama harufu ya divai ya Lebanoni. Efraimu atasema, Mimi nina nini tena na sanamu? Mimi nimeitika, nami nitamwangalia. Mimi ni kama mberoshi wenye majani mabichi. Kwangu mimi yamepatikana matunda yako.
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 81:6-10, 13, 16 (K) 10, 11

(K) Mimi ndimi Bwana Mungu wako, Sikiliza sauti yangu.

Maneno yake nisiyemjua naliyasikia.
Nimelitenga bega lake na mzigo,
Mikono yake ikaachana na kikapu.
Katika shida uliniita nikakuokoa. (K)

Nalikuitikia katika sitara ya radi;
Nalikujaribu penye maji ya Meriba.
Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya,
Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza. (K)

Usiwe na mungu mgeni ndani yako;
Wala usimsujudie mungu mwingine.
Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
Niliyekupandisha toka nchi ya Misri. (K)

Laiti watu wangu wangenisikiliza,
Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano,
Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani. (K)

SHANGILIO
Zab. 95:7, 8

Leo msifanye migumu mioyo yenu; Lakini msikie sauti yake Bwana.

INJILI
Mk. 12:28-34

Mmojawapo wa waandishi alifika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza.
Yesu akamjibu, ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Yule mwandishi akamwambia,Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia. Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MASOMO YA MISA: Ijumaa, Juma la 3 la Kwaresima Mwaka A Tarehe 24/03/2017 Rating: 5 Reviewed By: Unknown