728x90 AdSpace

­
Latest News
March 8, 2017

JE, UMEKATA TAMAA? Mfahamu Mtu aliyekata tamaa na dalili zake- 2


Na. James J. Waibina
Mpendwa msomaji wa Jarida letu la Fumbuka na BLOG yetu ya Fumbuka kupitia fumbukasasa.blogspot.com, Nichukue fursa hii ya pekee kukukaribisha kwa mara nyingine katika makala hii ya KIJANA AMKA.

Baada ya kuangalia Maana ya Kukata  tamaa katika Makala iliyopita, leo tutaangalia dalili za ndani za mtu aliyekata tamaa hivyo karibu uwe nami ili uweze kujifunza mengi yamkini nawe umekata tamaa ila hujijui.

Hizi ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika hawawezi kuzitambua kiurahisi, ni muhusika tu ndiye anaweza kuzitambua au kuhisi, Sasa tuziangalie dalili hizi angalau kwa  undani zaidi.

1. Kukosa msukumo kimawazo.
Kwakua kila jambo linaanzia kwenye mawazo, ili mtu afanikiwe anahitaji msukumo na ushawishi wa mawazo yake.
Maana mawazo anayokuwanayo mtu kwa muda mrefu, huwa yanajitokeza katika maneno yake na hatimaye katika matendo yake.

Hivyo basi ukiona msukumo wa mawazo yako ya mwanzo umepungua, basi ujue kuwa hiyo ni dalili mojawapo ya kukata tamaa.

2. Kuhisi kuchoshwa kimawazo
Ukiona mawazo yako yamechoshwa kwa kuliwazia jambo fulani ambalo mwanzoni ulikuwa umelipanga vizuri, nayo ni dalili ya kukata tamaa.

3. Mawazo ya kushindwa (Hasi)
Haya ni mawazo ambayo siku zote hayana ushawishi wa kukusaidia kufanya jambo lolote, badala yake huleta woga kufanya jambo kwa kuhofia kushindwa au kukosa uhakika wa kufikia malengo.

4. Kukosa ubunifu wa njia mbadala
Ukiona jambo linashindikana kwa njia moja na huku unakosa ubunifu wa njia mbadala jinsi ya kulifanikisha jambo hilo, nayo inaweza ikawa ni dalili ya kukata tamaa. Kila mtu ana uwezo mkubwa sana wa ubunifu, tofauti zetu zinajitokeza pale ambapo wengine wanashughulisha sana sehemu ya ubongo zinazo husika na ubunifu, wakati wengine wamezilemaza.

5. Kupoteza furaha /hamu ya jambo husika.
Jambo ambalo ulikuwa unalifurahia na kuliona nzuri, huku ukifikiria kufikia mafanikio, ghafla unaanza kupoteza furaha au hamu ya jambo hilo, nayo ni moja ya dalili ya kukata tamaa.

6. Kutofurahia ushauri
Ukiona unaanza kuchukia ushauri hasa unaokwenda kinyume na mawazo yako au ushauri unaokushawishi kuendelea kufanya jambo ambalo umeamua kuliacha. Hii inaweza kuwa dalili ya kukata tamaa.

7. Kufanya maamuzi ya haraka
Mawazo yako yanapoamua kufanya maamuzi yanayohatarisha maafanikio yako, au kuhatarisha maisha yako kama kujiua, ni dalili tosha ya kukata tamaa.

8. Kupoteza taswira ya mafanikio
Taswira ya mafanikio ndio msukumo halisi wa kufikia mafanikio. Kupoteza taswira ya mafanikio akilini mwako, ni dalili ya kukata tamaa.

9. Kupoteza ujasiri
Akili yako inapopoteza ujasiri juu ya jambo ambalo hapo mwanzo ulikuwa na ujasiri mkubwa wa kulitenda au kukabiliana nalo, hapo moja kwa moja utakuwa umefikia hatua ya kukata tamaa.

10. Kujihurumia
Hili nalo ni tatizo la ndani ya mtu, unapoanza kuona akili yako inajihurumia nakuona kama watu au jambo lina kukosesha furaha ni dalili ya kukata tamaa.

11. Kujihisi hufai kabisa
Unahisi maisha yako hayana jambo lolote la maaana la kuchangia na hayafai kabisa. Huenda ukahisi unahatia nyingi. Hii pia ni dalili ya kukata tamaa.

12. Kutamani kufa
Baadhi ya watu hutamani kufa kuliko kuishi kwasababu ya mambo ya hapa duniani yaliyowaumiza mioyo. Wengine hutamani kujiua na wengine hufikia hatua ya kumwomba Mungu awachukue kama vile nabii Elia katika biblia alivyoomba (1wafalme 19:4).

Kwa leo  tuishie hapo, katika Makala ijayo tutazungumzia Dalili za nje za mtu aliyekata tamaa.

******************************************

ITAENDELEA ........

Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia

0713515059  -(WhatsApp) au  jameswaibina@fumbuka.co.tz
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: JE, UMEKATA TAMAA? Mfahamu Mtu aliyekata tamaa na dalili zake- 2 Rating: 5 Reviewed By: Unknown