728x90 AdSpace

­
Latest News
March 10, 2017

Zifahamu Faida Za Kuwa Mbunifu Kwenye Biashara Yako


Na. James Waibina.
Karibu Mpenzi Msomaji na mfuatiliaji wa Makala zetu katika Blog hii ya Fumbuka..
Baada ya kuangalia mbinu za kukusaidia  kuwa mbunifu katika makala iliyopita, Leo katika Makala hii ya "Fursa kwa wote" ninakuletea Faida azipatazo Mtu aliye mbunifu katika biashara yake.

Ebu kwanza tujikumbushe maana ya Ubunifu, Ubunifu ni uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya au mbinu mpya za namna ya kukamilisha jambo fulani kwa ufanisi, au tunaweza kusema ubunifu ni ujuzi wa kuleta jambo lilelile kwa muonekano tofauti.

   Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako unahitajika uwe mbunifu sana, yani hakikisha leo yako ni tofauti na jana yako, kuwa mbunifu kila iitwapo leo kwenye biashara yako utafanikiwa sana, unaweza kuwa unafanya biashara sawa na watu wengine lakini kama wewe utakuwa mbunifu utaileta kwa muonekano tofauti ambao utawafanya watu wengi wakupende wewe,kuwa mbunifu kwenye biashara yako kutakuhakikishia mafanikio makubwa sana kwenye biashara yako.
    Faida azipatazo mtu aliye Mbunifu katika biashara ni pamoja na;-

    1.  Kuongeza Uwezo
     Mtu ambae ni mbunifu siku zote yeye huumiza kichwa sana kuhakikisha kuwa anakuja na kitu tofauti, hii humjengea uwezo mkubwa sana kwenye mambo yake, hivyo basi mtu mbunifu ana uwezo mkubwa sana kwenye biashara zake kuliko mtu ambae sio mbunifu kwasababu mtu mbunifu muda wote kichwa kinachakarika kuleta mawazo mapya.

   2.  Kuwa tofauti na wengine
      Faida ya kuwa mbunifu kwenye biashara yako ni kuwa tofauti na watu wengine. Siku zote kwenye maisha hauwezi kuwa sawa na wengine kama wewe ni mbunifu kuliko watu wengine, utakuwa watofauti tu hata kama watu watasema nini kuhusu wewe lakini mwisho wa siku wewe utaendelea kuwa mtu wa tofauti tu kwenye maisha yako, kiuchumi, kifikra na hata kimawazo kwa sababu ya ubunifu wako.
  
   3.  Kupunguza Ushindani
     Kama tunavyojua kuwa washindani ni wengi sana kwenye biashara yoyote ile, unachotakiwa kuwashinda washindani wako sio kugombana nao, sio kuwatukana hapana unachotakiwa kufanya hapo ni kuhakikisha wewe unakuwa mbunifu tu sana kwenye biashara yako, jinsi unavyokuwa mbunifu ndio unazidi kuwapunguza, kwasababu wao watajua kesho utakuwa vile vile kumbe kesho unakuja kivingine mwisho wa siku utawaacha mbali tu kimaisha kwasababu wewe ni mbunifu kuliko wao.
  
    4.  Kuongeza Masoko
    Faida nngineyi ya kuwa mbunifu ni kuhakikisha unapata masoko sana, nilishakwambia hapo mwanzo kuwa moja ya kitu kinachoweza kukufanya kupata masoko ni kuwa tofauti na huwezi kuwa tofauti kama sio mbunifu, jitahidi sana kwenye maisha yako, kuwa mbunifu utaona utakavyweza kupata masoko mengi ya kuuza bidha zako.

Hizo ndizo Faida azipatazo Mtu aliye Mbunifu katika biashara yake.

Ahsante.
Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia

0713515059  -(WhatsApp) au  jameswaibina@fumbuka.co.tz
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: Zifahamu Faida Za Kuwa Mbunifu Kwenye Biashara Yako Rating: 5 Reviewed By: Unknown