728x90 AdSpace

­
Latest News
March 25, 2017

TAFAKARI YA SIKU: Habari Kuu ya Historia ya Ukombozi wa Mwanadamu- (Tarehe 25/03/2017)




“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumamosi, Machi 25, 2017,
Juma la 3 la kwaresima
Sherehe ya Kupashwa habari ya kuzaliwa Bwana

Isa 7:10-14, 8:10;
Zab 40:7-11;
Ebr 10:4-10;
Lk 1:26-38

HABARI KUU YA HISTORIA YA UKOMBOZI WA MWANADAMU

Leo kanisa lina sheherekea tangazo la mapenzi ya Mungu ya kutaka kumuokoa mwanadamu. Kupashwa habari ni mwaliko wa kila mmoja kujazwa na furaha na shukrani, tunapo tafakari juu ya Upendo wa Mungu wakutuokoa sisi. Tunafurahi kuona kujitoa na kukubali kwa Maria. Inaonesha ni kwa jinsi ghani kusema ‘ndio’ kwa mapenzi ya Mungu inaweza kuleta tukio la pekee kabisa katika maisha yetu, kama Bikira Maria alivyosema ‘ndio’ na kuleta tukio la ukombozi wa wanadamu. Kwa ‘ndio’ hii sio kwamba tu mipango ya Mungu inafanya kazi, bali Mungu mwenyewe anakuja kukaa ndani yetu na kati yetu. 

Maria alionesha ni kwa jinsi ghani ya kuwa mfuasi wa Kristo, kwa kujikabidhi kwenye mikono ya Mungu anaye tupenda sisi. Wakati tunatafakari kama tunaweza kufanya kitendo hicho cha kujitoa kabisa na kujiweka katika mikono ya Mungu, tutambue kuwa wakati Mungu anatuita anatupatia pia neema. Kujikabidhi kwa Mungu, na kuacha yote na kujiweka mikononi mwake sio kitu rahisi. Ina maana kuacha mengine yapite, na kama Maria kuyakabili yale tusio yatambua kwa akili zetu ambayo yanatutisha. Mungu awezi kutupa kitu kama mikono yetu sio mitupu ili tuweze kupokea. Tukiwa tumekumbatia au kushika vitu mikononi hatuwezi kupokea vitu kutoka kwa Mungu. Sababu kwa nini kuna watakatifu wachache ni kwasababu hatutaki kumwachia Mungu atupende. Kupendwa maana yake, kujikabidhi kwa Mungu, kujikabidhi, kumtazama tu Mungu kwa Mungu bila kutegemea nguvu tofauti, na kutegemea yote jinsi Mungu anavyotaka. Maana yake ni furaha ya kukubali utupu wetu anayetoa yote, bila kuhesabu ni mangapi tunayompa kama zawadi. Sisi wote tunakabiliwa na utayari na uamuzi wa Maria. Je, tupo tayari kujikabidhi kwa Mungu na kumwomba Mungu afanya yale yote ambayo kwa jicho la kibinadamu tunaona hayawezekani? 

Sala: Mungu mwenyezi, tunakuomba sala za Maria zimlete Yesu kwa dunia. Yesu nakuamini wewe. Amina
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: TAFAKARI YA SIKU: Habari Kuu ya Historia ya Ukombozi wa Mwanadamu- (Tarehe 25/03/2017) Rating: 5 Reviewed By: Unknown