728x90 AdSpace

­
Latest News
March 8, 2017

JE, UMEKATA TAMAA? Mfahamu Mtu aliyekata tamaa na dalili zake.


Na. James J. Waibina

Mpendwa msomaji wa Jarida letu la Fumbuka na BLOG yetu ya Fumbuka kupitia fumbukasasa.blogspot.com Nichukue fursa hii ya pekee kukukaribisha katika makala hii ya FAHAMU, makala ambayo hukufahamisha masuala mbalimbali yahusuyo maisha na jamii yetu kwa ujumla.

Leo katika Makala hii ninakuletea Dalili za mtu aliyekata tamaa katika Jambo lolote maishani mwake hivyo karibu uwe nami ili uweze kujifunza mengi yamkini nawe umekata tamaa ila hujijui.

Awali ya yote ni vyema tukafahamu maana ya kukata tamaa..

MAANA YA KUKATA TAMAA
Kukata tamaa ni hali ya kupoteza matumaini, hari hii hutokea pale ambapo mtu amepoteza wazo au matumaini ya kufanikiwa katika matarajio yake ya kupata kitu fulani au kufanikiwa kwa jambo lolote alilopanga.

Pia ni kupoteza tumaini la kufikia malengo katika jambo fulani alilopanga kulifanya au analolifanya, ni hali inayoweza kutokea katika mfumo wa maisha ya kila siku, iwe nyumbani, Kazini, shuleni, kwenye biashara, katika mahusiano au mahali pengine popote katika mfumo wa maisha.

Hii ni hali ya kuchoshwa au kuvunjwa moyo kunakotokana na mtazamo hasi unaoweza kuujenga baada ya  kufikia Ukomo wa ufahamu, ufumbuzi au suluhisho la suala lolote linalokukabili, iwe kutokana na mawazo yako binafsi au mawazo ya yatokanayo na wengine.

Hili ni tatizo kubwa linalowafanya watu kutofikia malengo yao au kutopata mafanikio katika maisha yao ya kila siku.

Baada ya kuangalia Maana ya Kukata  tamaa, sasa tuangalie dalili za mtu aliyekata tamaa.

Kuna dalili nyingi za mtu aliyekata tamaa ambazo hutofautiana kutokana na mazingira, sababu, wahusika, matukio n.k.
Lakini zipo dalili za msingi na za jumla kwa watu wote. Dalili hizo tunaweza kuzigawa katika sehemu Kuu mbili ambazo ni:

(i) Dalili za Ndani

Hizi ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika hawawezi kuzitambua kiurahisi, ni muhusika tu ndiye anaweza kuzitambua au kuhisi.

(ii) Dalili za Nje

Hizi ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika tunaweza kuwa mashahidi kwa kuziona kwa uwazi na kutambua kwamba mwenzetu amekata tamaa.

Sasa tuziangalie dalili hizi angalau kwa undani zaidi.

DALILI ZA NDANI ZA MTU ALIYEKATA TAMAA

1. Kukosa msukumo kimawazo.

Kwakua kila jambo linaanzia kwenye mawazo, ili mtu afanikiwe anahitaji msukumo na ushawishi wa mawazo yake.
Maana mawazo anayokuwanayo mtu kwa muda mrefu, huwa yanajitokeza katika maneno yake na hatimaye katika matendo yake.

Hivyo basi ukiona msukumo wa mawazo yako ya mwanzo umepungua, basi ujue kuwa hiyo ni dalili mojawapo ya kukata tamaa.

2. Kuhisi kuchoshwa kimawazo

Ukiona mawazo yako yamechoshwa kwa kuliwazia jambo fulani ambalo mwanzoni ulikuwa umelipanga vizuri, nayo ni dalili ya kukata tamaa.

Kwa leo tuishie hapo.....

*****************************************

ITAENDELEA ........

Imetayarishwa na:   James J. Waibina

Kwa Maoni /Ushauri: Tuwasiliane kupitia

0713515059  -(WhatsApp) 
             au 

MBARIKIWE.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: JE, UMEKATA TAMAA? Mfahamu Mtu aliyekata tamaa na dalili zake. Rating: 5 Reviewed By: Unknown