Na Daniel
Makaka- Sengerema.
Mkuu wa
wilaya ya Sengerema,mkoani Mwanza, Bi Kalen Yunus amekifunga chuo cha uuguzi
cha Huruma ya Mungu Yatosha baada ya kukiukwa kwa taratibu za usajili.
Mkuu huyo
aliamua kukifunga chuo baada ya kupata taarifa za chuo hicho kuendeshwa bila
usajili.
Pamoja na
kufungwa kwa chuo hicho, wanafunzi wake wanaiomba serikali iwasaidie
kurejeshewa fedha walizotoa katika chuo hicho kutokana na mwenye chuo
kuwadanganya kuwa kimesajiliwa wakati akijua si kweli.
Wamesema
walijiunga hapo baada ya kuona matangazo mbali mbali kuhusu chuo hicho kuwa
kinatoa mafunzo ya uuguzi na maabara na kwamba inachukua watu wa kidato cha nne
bila kujali matokeo.
Jengo la
chuo feki cha Uuguzi (nursing) cha Huruma ya Mungu Yatosha kilichopo kata
ya nyehunge wilayani Sengerema.
|
Wamefafanua
kuwa baada ya kufika chuoni hapo , kata ya Nyehunge wilayani humo mazingira ya
chuo hicho yalikuwa na utata kutokana na kutokuwa na madarasa ya kutosha na
wakazi wa maeneo hayo kutokuwa na taarifa ya uwapo wa chuo hicho na
kuwashangaa wanafunzi hao.
Wamefafanua
kuwa baada ya kukaa kwa muda mfupi mabadiliko mbali mbali yalikuwa yanafanyika
katika chuo hicho huku wanafunzi wakifukuzwa pasipo utaratibu kitendo ambacho
kiliwatia shaka.
Aidha chuo
hicho kilikuwa na mwalimu mmoja tu aliyekuwa anafundisha tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2013.
.......Wanafunzi
wakiwa na majonzi ya baada ya kutapeliwa......
|
Kwa upande
wake mmiliki wa chuo hicho Bw, Ballu Clavery amekiri wazi kuwa chuo hicho
hakijasajiliwa na alitumia namba ya zahanati iliyokuwa inamilikiwa na mjomba
wake ili kuanzisha chuo hicho.
0 blogger-facebook:
Post a Comment