Kiongozi wa
Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amemtua askofu Joseph Kulola kuwa askofu
mpya wa Jimbo la Kigoma.
|
Akizungumza
na Radio Kwizera kwa njia ya simu kutoka wilayani Biharamulo mkoani Kagera,inakoendelea
awamu ya pili ya Sinodi kwa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Askofu Severine
Niwemugizi wa Jimbo hilo amesema uteuzi huo umefanyika Julai 10,2014 majira ya mchana.
Amesema
askofu huyo mteule ni mzaliwa wa Jimbo la Same, Mkoani Kilimanjaro ambaye kwa
sasa ndiye mkuu wa Seminari ya Mt Paul iliyoko Kipalapala Mkoani Tabora.
Askofu
mteule Kulola anayetokea Shirika la Kazi ya Roho Mtakatifu ameteuliwa kuchukua
nafasi ya aliyekuwa askofu wa Jimbo la Kigoma askofu Protas Rugambwa ambaye kwa
sasa yuko kwenye idara ya Uinjilishaji mjini Roma, Italia.
Habari
Na:-Radio Kwizera FM-Ngara.
0 blogger-facebook:
Post a Comment