MBUNGE wa Jimbo la Kasulu mjini Moses Machali anatuhumiwa kumtwanga baba yake mzazi Mzee Machali sambamba na kumfukuza nyumbani kwake,kutokana na kitendo chake cha kulewa kupindukia ambayo imekuwa adha kwa mbunge huyo na kupelekea mgogoro mkubwa baina yake na mzazi huyo.
Awali Julai ,15, 2014 usiku mzee alichelewa kurudi nyumbani na alipomgongea mwanae afungue mlango ndipo akapata kichapo kutoka kwa mbunge huyo baada ya kuona adha hiyo ni sugu kwa mzee wake.Akiongea kwa njia ya simu na mtandao huu mbunge huyo alisema mzazi wake anapenda kunywa pombe kupindukia hali inayomfanya kila wakati wagombane juu ya tabia hiyo ambapo kwa upande wa pili kisiasa inamuathiri katika uwajibikaji wake kwa wananchi.Alisema baba yake anatumiwa na chama cha ccm kwa lengo la kumdhoofisha kisiasa hasa katika kipindi hiki cha majeruhi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwakani na kumtaja balozi wa mtaa wa mwilavya Dickson Joaqim ni miongoni mwa watu wanaomshawishi mzee wake kituo cha polisi kumshtaki.
“sijafikia hatua ya kumpiga mzee wangu,najitambua ndio maana namsihi baba achane na pombe ambapo mimi najiskia vibaya kuona analewa sasa tukiwekana sawa baadhi ya watu wanadai nampangia sheria na ndo hivyo wanazusha ya kuzusha” alibainisha Machali.Alisema kwa kuthibitisha hilo umma kuwa hajampiga mzee wake na kwenye mkutano wa hadhara wilayani hapo, atakuwa sambamba na mzee huyo na kukiri mzee wake amefuta kesi dhidi yake na kusisitiza ccm watumie mbinu za ziada na kudai hawana jipya.Shuhuda mmoja jina kapuni akiri kumuona mzee huyo akiwa na `PF3′ akitembea kwa shida huku mkono wake ukiwa umevimba akipatiwa matibabu katika moja ya zahanati ya wilayani hapoAkithibitisha hilo Kamanda wa Polisi Mkoa Frasser Kashai alisema ni kweli mzee wake amefungua jalada la kumshataki mbunge huyo na wao wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kukamilisha taratibu za mashataka
0 blogger-facebook:
Post a Comment