Jeshi la Polisi nchini Kikosi cha Usalama Barabarani
limewafukuza kazi askari 27 baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya
rushwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza nidhamu, uwajibikaji na maadili
ya kazi kwa askari polisi wa barabarani nchini.
Askari hao wamefukuzwa kazi kuanzia Januari mwaka
huu ambapo uamuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa usimamizi wa nidhamu na
mapambano dhidi ya rushwa baada ya baadhi ya askari wa jeshi hilo kudaiwa
kujihusisha zaidi na vitendo hivyo.
Ni katika mkutano na waandishi wa habari ndipo
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga anasema
usimamizi huo dhidi ya vitendo vya rushwa umesaidia ongezeko la ukamataji wa
makosa na mabadiliko ya nidhamu za madereva kwenye matumizi ya barabara.
Akatoa tathmini ya ajali za barabarani na kubainisha
Mikoa iliyoongoza kwa ajali nyingi kuanzia Januari mwaka huu ni Dar Es Salaam
yenye ajali 5,052 Morogoro ajali 514 huku Kilimanjaro ikiwa na ajali 332.
0 blogger-facebook:
Post a Comment