Muigizaji mwanamke nchini Marekani aliyemtumia Rais Barack Obama barua iliyokuwa na sumu ya Ricin amefungwa jela kwa miaka 18.
Shannon
Richardson, mwenye umri wa miaka 36, kutoka Texas, pia alimtumia meya wa
New York Michael Bloomburg barua nyingine iliyokuwa na sumu hiyo hiyo. Alidai kuwa mumewe waliyeachana naye ndiye alituma barua hizo katika njama ya kumlimbikizia madai hayo.
"sikuwa na nia ya kumdhuru mtu'' Shannon aliambia mahakama.
Alikiri kosa la kumiliki na kutengeza sumu hiyo mwezi Disemba.
Jaji alimpa hukumu kubwa zaidi ikilinganishwa na kosa lake na pia kutakiwa kulipa faini ya dola 367,000.
Richardson, mama mwenye watoto six, ameigiza katika vipindi kama 'The Vampire Diaries' na 'The Walking Dead.'
Viongozi
wa mashitaka wanasema kuwa mwanamke huyo aliagiza bidhaa za kutengeza
sumu hiyo kupitia kwa mtandao kisha akatuma barua tatu zilizokuwa
zimepakwa sumu hiyo.
Shannon mwenye watoto sita aliomba mahakama kumhurumia kwa kumpa adhabu ndogo
Kulingana
na viongozi wa mashitaka, moja ya barua alizomtumia Obama , ilikuwa na
maandihsi haya: "kilicho ndani ya barua hii, hakiwezi kulinganishwa na
mipango yangu kwako bwana Rais. ''
Barua
nyingine iliyopokewa na meya Bloomberg, anayeunga mkono kudhibitiwa kwa
bunduki, ilisema, '' mpige risasi mtu yeyote atayekuja kuchukua bunduki
za mtu aliyetuma barua hii.''
Barua ya
tatu iliyokuwa na kemikali hiyo ya sumu, ilifunguliwa na bwana Mark
Glaze, mkurugenzi mkuu wa idara inayofadhiliwa na Meya ya kupambana na
silaha haramu.
Richardson katika kumtaka jaji kumhurumia, aliomba msamaha akisema, '' mimi sio mtu mbaya. Sina nia ya kumdhuru mtu yeyote.
Aliomba msamaha na huruma na kusema tayari anahisi ameadhibiwa vya kutosha kwa kunyang'anywa watoto wake sita
Betting in your city - Sporting 100
ReplyDeleteBetting septcasino.com in bsjeon.net your 토토사이트 city novcasino - Sporting 100 communitykhabar