Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) na kupokelewa na Ndg. Felix Maagi Kaimu Mkurungenzi Mkuu NHC na Mkurugenzi wa Fedha kulia wakati alipokagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya kikazi jana Rais Dr. Jakaya Kikwete anaendelea na ziara mkoani humo leo.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa shirika la Nyumba wakati alipowasili katika eneo la mradina kujionea shughuli za ujenzi katika mradi huo
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizindua mradi huo pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Felix Maagi na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene kulia na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi kwa pamoja wakipiga makofi mara baada ya Rais kuzindua rasmi mradi huo uliopo wilayani Mkinga
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisikiliza kwa makini wakati akipata maelezo ya mradi huo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. elix Maagi.
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Rais Dr. Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa wa pili kutoka kushoto , Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. George Simbachawene wa pili kutoka kulia na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Rais jakaya Kikwete akikata utepe kabla ya kukabidhi Mashine za kufyatulia matofali kwa mkuu wa mkoa wa Tanga ambazo zitagawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa Tanga mashine nne kulia ni mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Chiku Galawa.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akipata taarifa ya mradi huo wa nyumba za gharama nafuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. Felix Maagi
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana
0 blogger-facebook:
Post a Comment