Wakizungumza na Wana Habari wananchi hao walisema kuwa kutokana na kituo hicho kutokuwa na Chumba cha kuhifadhia maiti wameiomba bodi ya Afya ili kusaidia ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti, kuondoa adha wanayokumbana nayo ya kushuhudia maiti zikilazwa kwenye vitanda vya wagonjwa.
Mmoja wa Wananchi hao, Sebastiani Katunzi alisema wanapopata msiba katika
hospitali hiyo wanakumbana na changamoto nyingi, kwani maiti zinalazwa kwenye
vitanda vya wagonjwa jambo linalowatia wasiwasi wagonjwa waliopo wodini.
“Tumeiomba bodi ya afya wilayani hapa isaidie kujenga chumba cha
kuhifadhia maiti, kwani watu tunapopata misiba tunakuwa na wasiwasi, kwani
tunashuhudia maiti zikilazwa kwenye vitanda vya wagonjwa jambo ambalo siyo
jema,” alisema Katunzi
Mganga Mkuu wa kituo hicho, Alobogasti Nkabyemanyira alisema kituo hicho
cha afya Morongo tangu kianzishwe wagonjwa waliokuwa wanalazwa walikuwa ni
wachache, hivyo ingetokea mgonjwa akafariki alikuwa anasafirishwa siku hiyo.
Nkabyemanyira alikiri kuwapo kwa tatizo hilo la kutokuwa na chumba
cha kuhifadhia maiti na kueleza kwamba wagonjwa wameongezeka kiasi
kikubwa na kusababisha kuwapo kwa upungufu wa vitanda pia.
“Ni kweli kuna tatizo, lakini tutawasilina na uongozi wa wilaya ili
bajeti ya mwaka ujao iweze kukidhi mahitaji kama hayo,” alisema Dk
Nkabyemanyira
0 blogger-facebook:
Post a Comment