728x90 AdSpace

­
Latest News
September 1, 2014

WELBECK AUZWA ARSENAL KWA PAUNI MILIONI 16 …apewa mkataba wa miaka mitano kukipiga.


MAMBO yanazidi kunoga katika dakika za lala salama kabla dirisha la usajili halijafungwa – Arsenal wanakamilisha usajili wa Danny Welbeck kutoka Manchester United kwa pauni milioni 16.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England ameafikiana na Arsenal kuhusu maslahi yake binafsi na atasaini mkataba wa miaka mitano kukipiga Emirates.

Klabu hizo mbili pinzani zimefikia makubaliano ya kufanya biashara ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 na kuzima njozi za Tottenham ambayo nayo ilikuwa ikisaka saini ya mkali huyo.
Welbeck atatangazwa rasmi kama mchezaji wa Arsenal muda mfupi ujao mara baada ya kufuzu vipimo vya afya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: WELBECK AUZWA ARSENAL KWA PAUNI MILIONI 16 …apewa mkataba wa miaka mitano kukipiga. Rating: 5 Reviewed By: Unknown