728x90 AdSpace

­
Latest News
September 10, 2014

MWANAMKE ADONDOKA KWENYE BODABODA NA KUKANYANGWA NA LORI: Tunaomba radhi kwa picha hizi===>

Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amekufa papo hapo baada ya kudondoka kwenye pikipiki aliyokuwa amepanda na kisha kukanyagwa na gari.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana  mchana katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tangibovu ambapo gari likiendeshwa na dereva asiyefahamika akitoka kwa Alysykes kuingia barabara ya Bagamoyo, aliigonga pikipiki namba T 505 CTJ Fekon ikiendeshwa na dereva asiyefahamika.
 
Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mbezi Makonde kwenda Mwenge ilikuwa imempakia mwanamke huyo ambaye baada ya pikipiki kugongwa alianguka chini na kisha kukanyagwa na lori namba T 277 CIL aina ya Tata likiwa na trela namba T 339 CYB lililokuwa katika uelekeo mmoja na pikipiki. 
 
Kamanda alisema mwanamke huyo alikufa papo hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala huku Polisi wakiendelea kuwasaka madereva waliohusika katika ajali hiyo.
 
KWA HABARI ZAIDI UNGANI NASI KWA KU-LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK.. Bonyeza hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MWANAMKE ADONDOKA KWENYE BODABODA NA KUKANYANGWA NA LORI: Tunaomba radhi kwa picha hizi===> Rating: 5 Reviewed By: Unknown