728x90 AdSpace

­
Latest News
September 5, 2014

AJALI YAUA ZAIDI YA 30 LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI


Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao ni Waandishi wa Habari mkoani Mara Frolence Focus wa Mwananchi na Pendo Mwakembe wa Raia Tanzania wamenusulika kwenye ajali hiyo wakiwa kwenye basi la Mwanza Coach kutokea Musoma. 
 




Mashuhuda wamesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 5 asabuhi, baada ya basi la Mwanza Coach lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la J4 lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Sirari. 






Zaidi ya watu 45 wanasadikiwa kufariki dunia na wengine wengi wakijeruhiwa vibaya baada ya mabasi mawili kugongana na kupinduka katika eneo la Sabasaba nje kidogo ya mji wa Musoma, mkoani Mara.




Wamesema mabasi hayo ambayo yote yalikuwa kwenye mwendo kasi yalikutana kwenye daraja dogo katika eneo hilo huku pia gari dogo aina ya Land Crusser likitaka kuovateki na hivyo kupelekea kutokea kwa ajali hiyo. Mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Nyamhanga amesema alisikia kishindo kikubwa muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na baadae kusikia vilio vikitokea ndani ya mabasi hayo. 




Mwenyezi Mungu azilaze roho za maremu wote mahala pema peponi..


Akizungumzia kwa tabu akiwa amelazwa kwenye wodi namba 4 hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara, Frolence amesema walishangaa kuona abiria waliokuwa wamekaa mbele wakisimama na kurudi nyuma na ghafla akasikia mlio mkubwa. 


Akizungumza nje ya chumba cha (ICU) kwa niaba ya Mganga Mkuu, Dakatari Martini Khani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa wamepokea idadi kubwa ya maiti na majeruhi huku idadi kamili ikiwa bado haijafahamika.


Jiunge nasi kwa kupata habari mpya zaidi Bonyeza hapa 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: AJALI YAUA ZAIDI YA 30 LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown