728x90 AdSpace

­
Latest News
September 5, 2014

KUKU WA KISASA WADAIWA KUSABABISHA UGONJWA WA KANSA

Kuku-June21-2014 c2eb0
Na Hudugu Ng'amilo   KUTOKA   NIPASHE ;
 
Ulaji wa kuku wa kisasa au broila' umeelezwa na wataalamu kuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maradhi ya saratani nchini.
Kitoweo hicho kinasababisha kansa kwa vile ndege hao hulishwa vyakula kama karanga, mahindi, mashudu na dagaa ambazo vina sumu ya 'mycotoxin' inayotokana na fangasi ambayo inachochea ukuaji wa seli za saratani mwilini.
 
Mshauri wa Mifugo wa kampuni ya Bytrade Tanzania , Omari Magoma, alitoa tahadhari hiyo katika mahojiano maalum ya NIPASHE Jumamosi, kuhusu ugonjwa huo na kufahamisha kuwa tatizo la kansa ya kuku linaendelea kuongezeka kila siku lakini likiwashambulia walaji na kukuza ukubwa wa kansa nchini.
Alisema ugonjwa huo ambao upo kwa muda mrefu kwenye miili ya kuku unasambaa sehemu zote mwilini mwake na pindi mlaji anapokula kitoweo hicho mara nyingi anaambukizwa maradhi ya kansa.
 
"Sumu ya mycotoxin huzalishwa na fangasi kutoka kwenye chakula kama mahindi, mashudu, karanga na dagaa vyakula ambavyo wafugaji huwalisha kukua ," alisema.
 
JAMII ZA FANGAS
Alibainisha kuwa, sumu hizo zina tabia tatu ambazo kusababisha kansa, kupunguza uwezo wa kuku kujikinga na maradhi ya kuambukizwa na kusababisha kuzaa viumbe wa ajabu.
Magoma alitaja fangasi hao kuwa ni aspegilus wenye sumu ijulikanayo kitaalamu kama aflatoxins b1 inayopatikana kwenye mahindi, mashudu, karanga na dagaa.
 
Aina nyingine ya fangasi ni 'penicillium' ambao wana sumu iitwayo ochratoxin A. Japo fangas hawa wanatengeneza dawa kama peniciline au PPF ambayo hutibu maradhi mengi wana sumu wanapotumiwa kwa utaratibu huo.
Fangasi wengine kwa mujibu wa Magoma ni fussanum wenye sumu ya fumonisins T-2 hawa ni jamii ya fangas wanaoonekana kwenye nafaka zikiwamo mahindi mchele na mtama.
 
UAMBUKIZAJI SARATANI " Kuku akila sumu hizi hupata kansa, kwa hiyo mwanadamu anaambukizwa kutokana na mabaki ya sumu hizo zilizo kwenye mwili wa kitoweo hicho na ataupata ugonjwa atakapokula mara nyingi nyama ya kukua" alionya.
 
Magoma alisema sumu hizo hupatikana katika mazingira ya uzalishaji kama joto, unyevunyevu unaoonekana kwenye mazao kuanzia utayarishaji mashambani hadi matumizi majumbani.
Aidha, kutokana na ukubwa wa tatizo mtaalam huyo aliwashauri wafugaji kutumia dawa ya mycotoxin binder au check-o-tox inayokamata sumu na kuitoa kupitia njia ya choo.
 
Alisema moja ya kazi ya kirutubisho hicho ni kudhibiti sumu hiyo, kupunguza unyevu kwenye chakula na huikusanya sumu kwenye mwili wa kuku kisha kuitoa kwa njia ya haja.
Pia aliwashauri wafugaji kununua vyakula vya kuku kwenye kampuni zinazozalisha kwa viwango na wale wanaotengeneza wahakikishe wanaweka kirutubisho hicho ili kukabiliana na tatizo la kansa ya kuku.
 
Magoma alitaja dalili za ugonjwa huo kwa kuku kuwa ni mifuu yao kuwa na madoadoa ya njano, ini lake kuwa kubwa zaidi na huwa na uvimbe kwenye utumbo.
 
MFUGAJI AZUNGUMZA Mfugaji wa kuku mkazi wa jijini Dar es Salaam, Jonesia John alisema kutoka aanze ufugaji kuku wake wamekuwa wakisumbuliwa na mafua ambayo yamekuwa yakiwasababishia kuwepo kwa idadi kubwa ya kifo.
Alisema ugonjwa mwingine ambao umekuwa ukiwasumbua kuku wake ni homa ya tumbo.
 
Kuhusu kansa ya kuku, alisema amekuwa akisikia wafugaji wenzake wakilalamikia hilo lakini hajawahi kushuhudia kuku mwenye nao.
Hata hivyo, alipoulizwa kama ana elimu yoyote ya ugonjwa huo ili pindi mifugo yake itakapopata aweze kukabiliana nao, alisema mara nyingi amekuwa akinunua vyakula salama vya kuku kwenye kampuni.
 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: KUKU WA KISASA WADAIWA KUSABABISHA UGONJWA WA KANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown