728x90 AdSpace

­
Latest News
August 25, 2014

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.
Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO Rating: 5 Reviewed By: Unknown