728x90 AdSpace

­
Latest News
August 18, 2014

UKATILI MWANAMKE AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO..

Mke wa mtu, Mwajuma Prima akiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
 
 Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini hapa. 


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.


Mama mdogo wa Mwajuma Prima akimuuguza mwanaye.
 “Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.

“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya? 

“Mabishano yalishika kasi na mwishowe walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa, akaingia jikoni na kuipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka na kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mume wa Mwajuma Prima akiwa na mama mdogo wa mwajuma.
 
 Akizungumza na gazeti hili, mama mdogo wa Mwajuma alisema: “Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana. 

“Fatuma alipoona kazidiwa aliingia jikoni akaipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia mwanangu mwilini na kumsababishia majeraha makubwa.”
Mume wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.”


Chanzo: Global Publisher.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: UKATILI MWANAMKE AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO.. Rating: 5 Reviewed By: Unknown