728x90 AdSpace

­
Latest News
August 25, 2014

MAUAJI: Al-Shabaab wamkata kichwa Mkenya, wateka magari mawili Kaunti ya Lamu


Watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa al-Shabaab waliuvamia msafara wa magari yaliyokuwa yakisafirisha mirungi kwenye Kaunti ya Lamu, na kumkata kichwa msaidizi wa dereva na kuyateka magari mawili, Kamishna wa Kaunti ya Lamu Miiri Njenga aliiambia Sabahi siku ya Jumatatu (tarehe 25 Agosti).

Njenga alisema magari hayo mawili yalikuwa yanasafirisha mirungi kuelekea Somalia kupitia Lamu pale yaliposhambuliwa kwenye msitu wa Bodhai wiki iliyopita. "Kulikuwa na watu wanne kwenye magari hayo wakati walipoamriwa kuingia msituni," alisema. 

"Watatu waliachiwa na watekaji nyara wao siku ya Jumanne (tarehe 19 Agosti). Mtu wa nne, jina lake kwenye kitambulisho chake ni George Mwiti kutoka Kaunti ya Meru, alipatikana amekatwa kichwa siku tatu baadaye." Mwili na kichwa vilipatikana kwenye eneo la Kiunga katika msitu wa Bodhai. 

Njenga alisema hakuna mali iliyoibwa na washambuliaji hao, ambao walijitambulisha kwa wahanga kama wanamgambo wa al-Shabaab.

 Chanzo: Sabahi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MAUAJI: Al-Shabaab wamkata kichwa Mkenya, wateka magari mawili Kaunti ya Lamu Rating: 5 Reviewed By: Unknown