728x90 AdSpace

­
Latest News
August 25, 2014

KAGAME CUP 2014:- El Merreikh waifunga APR 1-0 mbele ya Rais Kagame na kuwa Mabingwa wa Kagame CUP 2014.

Mchezaji wa Kimataifa wa Kenya, Allan Wanga, Leo Agosti 24,2014 huko Kigali, nchini Rwanda ameipa Timu yake ya El Merreikh ya Sudan Ubingwa wa Klabu za Afrika Mashariki na Kati na kutwaa Kagame Cup 2014, baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji APR waliokuwa wakishuhudiwa na Rais Paul Kagame kwenye uwanja wa Amahoro.

 Bao hilo la ushindi la Wanga lilifungwa katika Dakika ya 24 na kuwapa El Merreikh Kombe na kitita cha Dola 30,000.

APR imeambulia Dola 20,000 kwa kushika nafasi ya pili.

Mapema , Polisi ya Rwanda ilitwaa Nafasi ya 3 baada ya kutoka Sare 1-1 na KCC FC ya Uganda na kuiangusha kwa Penati 4-2 na kutwaa kitita cha Dola 10,000.

Mashindano hayo, ambayo hufadhiliwa na Rais Kagame, yalianza huko Kigali, Rwanda hapo Agosti 8,2014 na kushirikisha Klabu miamba ya Kanda hii ya Afrika.

Tanzania iliwakilishwa na Azam FC na KMKM ya Zanzibar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: KAGAME CUP 2014:- El Merreikh waifunga APR 1-0 mbele ya Rais Kagame na kuwa Mabingwa wa Kagame CUP 2014. Rating: 5 Reviewed By: Unknown