728x90 AdSpace

­
Latest News
August 28, 2014

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA


 Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekerege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.

Kadhalika, Ekerege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo. 

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.
Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown