728x90 AdSpace

­
Latest News
August 25, 2014

JAMAA MTU MZIMA ATIWA MBARONI KWA KUWALAWITI WATOTO WAWILI


JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Mhandisi Msose Michael (35) mkazi wa Mkaongo Juu Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuwalawiti mabinti wawili katika Kijiji cha Zogowale wilayani ya Kibaha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa huo, Athumani Mwambalaswa alithibitisha kukamatwa kwa mhandishi huyo na kusema aliwalawiti mabinti hao wenye miaka 12 na 16 kwa nyakati tofauti.

Alisema mtuhumiwa huyo aliwachukua mabinti hao kutoka Nachingwea kwa nyakati tofauti na kukaa nao nyumbani kwake jijini Dar es Salam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani.

Alisema baada ya siku kadhaa, aliwahamishia kwenye shamba lake lililopo Zogowale kwa ajili ya kutunza mifugo yake na kwamba alikuwa akilala nao chumba kimoja pindi alipowatembelea.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wananchi walioshuhudia kitendo hicho walitoa taarifa polisi ambao waliweka mtego na kumnasa mtuhumiwa huyo.

“Baada ya mtuhumiwa huyo kuwekwa chini ya ulinzi, mabinti hao ambao walipelekwa katika kituo cha afya Mlandizi kupimwa na kugundulika kwamba walilawitiwa hivyo kuanzishiwa matibabu,” alisema kamanda huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: JAMAA MTU MZIMA ATIWA MBARONI KWA KUWALAWITI WATOTO WAWILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown