728x90 AdSpace

­
Latest News
October 5, 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AMEFARIKI AKIWA NA NDOTO NYINGI ZA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA!



Watanzania wanaomboleza kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila, Mwenyekiti wa Chama cha DP, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jumapili tarehe 4 Oktoba katika kijiji cha Msolwa, Chalinze, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani akiwa anatoka Mkoani Njombe kuelekea Dar Es Salaam. 

Mchungaji Mtikila anakumbukwa na wengi kwa kusimama kidete kutetea demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania kunako miaka 1990. Mara kadhaa amefungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania na kushinda, ingawa maamuzi yake pengine hayakutekelezwa kutoka na mazingira ya kisiasa ya wakati wake. Ni kiongozi wa kwanza kisiasa nchini Tanzania kudai uwepo wa mgombea huru wa Urais, kwani hii ni haki ya watanzania kikatiba. Alidai pia uwepo wa Tanganyika. Ni kiongozi aliyetiwa mbaroni mara kwa mara na vyombo vya ulinzi na usalama.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 blogger-facebook:

Post a Comment

Item Reviewed: MCHUNGAJI MTIKILA AMEFARIKI AKIWA NA NDOTO NYINGI ZA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA! Rating: 5 Reviewed By: Unknown