Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisco, ya Jumatano, kwa mahujaji na wageni , alilenga zaidi katika Mkutano wa XIV, wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, ambamo alitoa wito kwa waamini wote, kiroho, waandamane na Mababa wa Sinodi kutafakari Wito na Utume wa Familia ndani ya Kanisa na Ulimwengu wa kisasa.
Amesema ni muhimu kwa familia kutembea katika njia ya Bwana, wakiushuhudia upendo wa Mungu na katika kuliwezesha Kanisa kutimiza utume wake katika dunia ya leo. Papa Francisco alielezea akilenga katika Mkutano wa Sinodi unaoendelea akisema , wajumbe wake wamezama katika tafakari ya kina juu ya wito na huduma ya Kanisa kwa jamii. Na hivyo, waamini wote wanahitajiwa kuungana na Maaskofu kupitia sala zetu na kimawazo pia. Papa ameutaja kuwa wakati huu ni wakati wa mchakato wa kina katika masuala yanayohusiana na Kanisa na familia, lengo lake zima na wazi linalotafutwa, ni kwa manufaa ya jumuiya yote ya Kikristo na binadamu wote.
Papa anasema ni wakati wa kutazama kwa makini maisha ya kila siku ya wanaume na wanawake wa leo, yenye kuonyesha haja ya kidharura inayohitajika kuimarisha roho familia. Papa ameonyesha kutambua ukweli wa hali halisi katika mahusiano kiraia, kiuchumi, kisheria, kitaalamu, kimbali, akisema mnahitaji kutumia kutumika hekima na busara, hasa katika mipangilio ya maisha yanayoonekana kuzongwa na ukame wa maisha, wenye kuleta mazingira magumu zaidi kwa familia husika .Kutokana na hili, ni jambo jema kwa pamoja kutazama mifumoipi inafaa kuzinasua familia hizo na hasa katika kupambana na hali halisi za kutelekezwa katika upweke na tatizo la wanandoa kupenda kuzaa watoto.
Hayo yanaigusa roho ya familia na kuwa sababu kwa nini Kanisa linahimiza familia zijifunue wazi kwa ajili ya jamii zima , kwa matazamio ya ubinadamu wenye kuchanua zaidi, na kufumbua macho zaidi ya vijana, kuona umuhimu wa mwendelezo wa maisha ya binadamu ndani ya familia. Na si hivyo tu lakini pia katika kujali mambo mengine yanayowakilisha maono ya uhusiano wa binadamu, kujengwa juu ya huru wa muungano wa upendo .Papa alisisitiza, Familia ni lazima itoe kipaumbele kama dhamana ya uaminifu, ukweli , imani, ushirikiano, heshima; katika moyo kuwa na ubunifu aminifu katika mahusiano ya kuaminiana, hata katika mazingira magumu. Na kwamba , Familia ni lazima iwe kioo cha maisha bora na kituo cha kufundisha heshima tangu katika kuzungumza kama mtu binafsi, na pia katika kuwa tayari kushirikishana mapungufu binafsi ya wengine.
Papa alieleza na kutahadharisha juu familia zinazoishi katika mazingira magumu zaidi, na hasa zilizo jeruhiwa kiroho na kihali , kama wale walioathirika na majanga ya asili katika mwenendo wa maisha yao. Papa alisema katika jamii, inayoziishi hali hizi , kwa hakika wanahitaji roho ya umoja wa kifamilia, ambayo haitokana na ushindani wala nia binafsi za kutaka kujulikana.
Hivyo Papa aliurejea Mkutano wa Sinodi akisema, kwa mtazamo huo, Kanisa linaitwa kutafakari kwa kina utume wake na kuchunguza kwa kiasi gani linaweza kuishi kama familia ya Mungu. Kama alivyosema Mtakatifu Petro, Kanisa linaitwa kuwa mvuvi wa watu, na hivyo pia linahitaji aina mpya ya wavu. Familia ni wavu huo. Familia ni wavu wenye kumweka mtu huru dhidi ya bahari ya upweke na kutelekezwa, na hivyo wote wanahaki ya kuishi kama watoto huru wa Mungu. Kanisa ni lazima litembee kwa kujiamini na kutweka nyavu zake kilindini ambako kuna samaki wakubwa. Na hili linawezekana kufanyika,
Papa alimalizia kwa kuomba Mababa wa Sinodi, waongozwe na Roho Mtakatifu, katika kulihamasisha Kanisa, kuweka nyavu zake nje wavu kwa kujiamini na imani katika neno la Mungu.
0 blogger-facebook:
Post a Comment